BARRICK GOLD CORPORATION YASALIMU AMRI KWA SERIKALI YA TANZANIA

  • Yakubali kampuni yake ya Acacia ilifanya makosa katika kuendesha shughuli zake nchini.
  • Ni baada ya kubainika kwa wizi wa madini katika makinikia na serikali kuzuia makontena yote bandarini, Mkuu wa Barrick alijitokeza na kuomba suluhu wayamalize.
RAIS MAGUFULI NA MWENYEKITI WA BARRICK
Rais, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation (Kampuni mmiliki wa Acacia) Prof. John L. Thornton ambaye alifika nchini tarehe 14 Juni, 2017 kukutana na serikali kuomba kufanya mazungumzo mazungumzo na kukiri kuwa Barrick Gold Mine iko tayari kulipa fedha zote ambazo Tanzania imepoteza kutokana na kampuni hiyo (Acacia) kuendesha shughuli zake hapa nchini.
  • Baada ya siku chache, timu ya viongozi waandamizi na wanasheria wa Barrick, walifika nchini tayari kwa mazungumzo na serikali.
  • Miezi michache baadae, makubaliano ya awali yalifikiwa na kusainiwa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
  • Na sasa nchi yetu, iko tayari kupokea fidia na malimbikizo ya kodi iliyokwepwa.
RAIS ASHUHUDIA BARRICK NA SERIAKALI WAKISAINI MAKUBALIANO
Rais Magufuli akishuhudia utiaji saini katika makubaliano ya awali baina ya Barrick Gold Corporation na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo;                                   a.) Wamekubali masharti yote yaliyopo katika sheria mpya ya madini zilizotungwa na Bunge na watahakikisha masharti hayo yanaingia kwenye mfumo wa fedha ambao wamekubaliana.                                                                        b.) Wamekubali serikali itapata hisa katika migodi hiyo kwa asilimia 16 kama sheria ilivyotaka, lakini pamoja na kumiliki migodi hiyo kwa asilimia 16 lakini kwenye mgao itakuwa nusu kwa nusu.      c.) Migodi hiyo itaweka fedha zinazotokana na madini katika akaunti zilizopo hapa nchini Tanzania.                       d.) Ofisi zao za London na ofisi zao za Johansburg katika siku za usoni, zitahamishiwa Tanzania na makao makuu ya kampuni hiyo yawe Mwanza ingawa wanaweza kuwa na ofisi nyingine sehemu nyingine nchini.                                   e.) Kuanzisha kampuni nyingine ya kusimamia na kuendesha migodi na makao makuu yake yatakuwa Mwanza na itaongozwa na mtendaji Mkuu, Mkurugenzi wa fedha na Mkurigenzi wa manunuzi kutoka Tanzania; Na ingawa serikali itakuwa na silimia 16 na mgao wa 50/50 wamekubali serikali itakuwa na wawakilishi katika bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo katika kila mgodi.     f.) Sehemu kubwa ya kazi zitolewazo mgodini sasa kwa kiasi kikubwa inavyowezekana zitafanywa na kampuni za kitanzania na Watanzania                                 g.) Kuimarisha huduma za jamii katika maeneo yaliyo karibu na migodi.                h.) Kila kampuni inayoendesha mgodi kuhakikisha inaachana na utaratibu wakutumia wafanyakazi wa mikataba na badala yake kuajiri wafanyakazi wa kudumu ambao ni wazawa na hawatakaa katika makambi ila kwenye makazi na familia zao, na watajenga barabara ili wafanyakazi waweze kutoka kazini na kwenda makwao.                     i.) Kuajiri Watanzania katika nafasi muhimu na za utaalamu, moja kwa moja au kuwafundisha ili baadae waweze kujaza nafasi za uongozi.                                      j.) Kutenga bajeti maalumu kwa ajili ya kuchangia utafiti wa kuendesha utafiti wa kuanzisha kiwanda cha kuchakata makinikia na kujenga maabara kubwa ya kupima makinikia.      k.) Serikali itakuwa na umiliki wa madini yote (rare metals) kama zitapatikana.            l.) Kesi zote na mashauri yote yatafanyika hapa Tanzania na sio nje kama ilivyokuwa zamani.                                      m.) Suala la fidia lilikuwa gumu sana na ndilo lililochukua muda mrefu na kusababisha kupitia nyaraka, ila BARRICK wamekubali kutoa USD Milioni 300 wakati mazungumzo ya jambo hilo yanaendela.

 

Mhe. Prof. Paramagamba Kabuni, Waziri wa Sheria na Katiba alisema,      “Watanzania tuna kila sababu ya kusema tumepiga hatua kuliko wale waliotutangulia katika jambo hili (Majadiliano kati ya Seriakli ya Tanzania na kampuni ya Barrick Gold Corporation) Na kwa hali hiyo kabisa nirudie tena, nimshukuru tena Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.. kwa lugha ya mtaani kwa ‘kuliamsha hili dude’. Baada ya hili dude kuamka, ambalo lilianzia kwenye makinikia.., na watu wengi walidhani issue yetu ni makinikia.. sisi tulivyokwenda kwenye majadiliamno tulikuwa na mambo makuu matano.. nje ya makinikia. Lengo letu lilikuwa kuyatumia mazungumzo haya kama alivyotuelekeza mwenyewe Mhe. Rais.. kufungua mwelekeo mpya wa usimamizi wa maliasili ya nchi yetu ikiwemo madini. – Profesa Paramagamba Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria

Tazama video

Ad

 

fuatilia hotuba ya Rais Magufuli akipokea ripoti ya mchanga wa madini

Ad

Unaweza kuangalia pia

SHERIA YA KODI YATOA MSAMAHA KWA MAPATO YASIYOZIDI MILIONI 4 KWA MWAKA

Na. Josephine Majura na Saidina Msangi, WFM, Dodoma Serikali imeeleza kuwa Sheria ya Kodi imetoa …

2 Maoni

  1. laurent pius katte

    Ni jambo la kujivunia nawapongeza viongozi wetu wote waliosimamia swala hili kwa uaminifu na umakini wa hali ya juu Mhe. Rais John Pombe Magufuli nakuombea kwa mungu akulinde na ma waziri na wengine wote na mimi binafsi lilikua likiniumiza roho sana

  2. Nampongeza Rais wa Tanzania J.P.Magufuli na kuwapongeza wote walosimamia jambo hili kwa msimamo mmoja bila kurudi nyuma na hatimaye kuleta natija nzuri ya mafanikio.Hongereni saana.Tunamatumaini makubwa sana kwa umoja wenu huu Nchi yetu itajikomboa na mabepari wanyonyaji wasiokuwa na huruma na mali ya Wananchi.Mungu Ibariki Tanzania, wabariki watu wake wote, waongoze wawe wamoja daima, waijenge Tanzania kwa manufaa ya wote.Ameen

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.