UFAFANUZI WA UDAHILI WA WANAFUNZI MWAKA WA KWANZA CHUO KIKUU DAR ES SALAAM.

MAHOJIANO KWENYE JAMBO TANZANIA (TBC1)
Naibu Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Prof. Bonaventure Rutinwa akihojiwa na mtangazaji wa kipindi cha asubuhi cha Jambo Tanzania kwenye Televisheni ya Taifa TBC1 bwana Mbozi Katara. Prof. ili kutoa ufafanuzi wa kile kilichoitwa mkanganyiko wa udahili wa wanafunzi wanaotakiwa kujiunga na masomo ya mwaka wa kwanza katika chuo hicho kwa mwaka wa masomo 2018/19.
  • Ni ule wa kufutiwa kuchaguliwa kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza 2018/19 zaidi ya 680.
  • Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – Taaluma Prof. Bonaventure Rutinwa atoa ufafanuzi. Fuatilia katika video hii

  • Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako atoa maelekezo kwa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kuhakikisha wanafunzi wote 682 waliofutiwa kuchaguliwa kwao warejeshewe nafasi zao na tayari uongozi wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam umewapa taarifa rasmi wanafunzi wote hadi usiku wa siku ya Jumatatu tarehe 22 Oktoba, 2018.
PROF. JOYCE NDALICHAKO, WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI
Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako ametoa maelekezo kwa chuo kikuu UDSM na TCU kuhakikisha wanafunzi wote 682 waliofutiwa nafasi za kujiunga na masomo ya mwaka wa kwanza chuoni hapo wanarudishwa kwenye orodha.
  • Maamuzi ya kikao cha dharula baina ya Mhe. Waziri, UDSM na TCU  ulikipa Chuo Kikuu UDSM kuongeza muda zaidi wa udahili. UDSM imeongeza wiki moja kwa wanafunzi wapya kutuma maombi yao ikiwa ni kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwamba kila mwanafunzi awe na uhuru wa kuchagua chuo anachokipenda kusoma na suala la udahili lishughulikiwe na chuo husika.  Tazama video ya maamuzi ya Prof. Nalichako katika link hii                                                                                                                                                                                    https://youtu.be/RAail7n-IqI

#SisiNiTanzaniaMpyA+

#MATAGA

Ad

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

TRA – WAFANYABIASHARA MSIJIHUSISHE NA BIASHARA ZA MAGENDO

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara na wachuuzi wanaoishi jirani na fukwe za Bahari …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *