- Ni raia wawili wa Afrika ya Kusini.. wapelelezi watambua majina yao na walipokuwa wakiishi jijini Dar es Salaam kwa muda wa miezi kadhaa.
- Walifikia hotel ya Whitesands na kisha kupanga nyumba eneo la Mbezi Beach kama wafanyabiashara wa Madini.
- Nyumba na chumba waliomfungia mfanyabiashara huyo wapelelezi mahiri wa vyombo vya ulinzi, waibaini! Iko Mbezi Beach mtaa wa Mwansasu.
- Ni nyumba ya marehemu Mwansasu inayomilikuiwa na binti zake kwa sasa.
- Dereva Taxi (taxi bubu) bwana Twalib Mussa anayefanyia shughuli zake eneo la White Sands Hotel ndiye aliyehusika kuwapangisha nyumba hiyo kwa bei ya USD 1,500 kwa mwezi kwa mgawanyo wa wenye nyumba wapate USD 1,300 na yeye kama dalali apate USD 200.
- Dereva huyo ndiye aliyeendesha gari lenye namba T918 CCY Toyota Mark II GX 110 Grande lililowabeba wahusika kutoka eneo la Gymkhana baada ya kumtelekeza mfanyabiashara MO na gari lililotumika kumteka.
- Dereva Taxi bubu huyo amekiri baada ya kutoka Gymkana, aliwapeleka wahalifu hao kituo cha mabasi ya mkoani eneo la Ubungo ili watoroke kwenda nje ya jiji la Dar es Salaam.
- Jeshi la polisi bado linaenendelea na upelelezi wa tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji MO.
Fuatilia maelezo ya Kamanda Mambosasa na dereva aliyetumika kuwapangisha kisha kuwatorosha watekaji;
Ad