Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Teminal 1 wakati akijiandaa kurejea nchini Rwanda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili jijini Dar es Salaam.

RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU MBILI NCHINI

Screen Shot 2019-03-08 at 1.47.45 PM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati akimsindikiza kwenda kupanda ndege katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
  • Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Paul Kagame  tarehe 08 Machi, 2019 amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku 2 hapa nchini Tanzania na kurejea nchini kwake, baada ya hapo jana kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
RAIS MAGUFULI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati akimsindikiza kwenda kupanda ndege katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
  • Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Mhe. Rais Kagame ameagwa na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli.
RAIS MAGUFULI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
  • Mara baada ya kuagana na mgeni wake, Mhe. Rais Magufuli amesalimiana na wananchi wa Dar es Salaam waliojitokeza kumuaga Mhe. Rais Kagame ambao wengi wao walikuwa ni wanawake na kuwatakia heri ya Siku ya Wanawake ambayo huadhimishwa tarehe 08 Machi, kila mwaka duniani kote.
RAIS MAGU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na vikundi mbalimbali vya ushehereshaji katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kumsindikiza mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame.
  • Katika salamu hizo, Mhe. Rais Magufuli amewashukuru wanawake wote hapa nchini kwa mchango wao mkubwa kwa Taifa na amesema Serikali inatambua na kuthamini juhudi zao mbalimbali.
Screen Shot 2019-03-08 at 1.33.46 PM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na vikundi mbalimbali vya ushehereshaji katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kumsindikiza mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame.
  • “Mungu awabariki sana akina Mama, mnafanya kazi nzuri kwa ajili ya Taifa hili, endeleeni kuimarisha umoja wa Watanzania wote, Serikali ninayoiongoza inathamini sana kazi nzuri zinazofanywa na akina Mama, endeleeni kutembea kifua mbele, Mungu atawalinda, na mimi sasa hivi naondoka kwenda kumuona Mama yangu hospitalini katika siku yake hii, pia natoa shukrani nyingi kwenu na kwa viongozi wa Mkoa na Wilaya kwa jinsi mnavyojitolea kuwapokea na kuwaaga vizuri wageni wetu” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *