JUMUIA YA WATOA HUDUMA YA MAFUTA NA GESI NCHINI, WAKUTANA NA WAFANYABISHARA WA GESI NA MAFUTA NCHINI BRAZIL

  • Ujumbe wa wafanya biashara pamoja na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mashirika ya serikali kutoka Tanzania ikiongozwa na mkuu wa msafara Balozi Abdulsamad Abdulrahim ambae pia ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Mafuta na Gesi nchini, na Makamu wa Rais na watendaji wakuu wa kampuni ya mafuta na gesi ya Brazil Petrobras wamekutana Nchini Brazil kwa mazungumzo ya mashirikano kati ya pande hizo mbili. Mazungumzo hayo yalifanyika  makao makuu ya kampuni hiyo jijini Rio de Janeiro.
BZ
Ujumbe wa Wafanya biashara pamoja na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mashirika ya Serikali kutoka Tanzania ikiongozwa na mkuu wa msafara Balozi Abdulsamad Abdulrahim ambae pia ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Mafuta na Gesi nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais na watendaji wakuu wa kampuni ya mafuta na gesi ya Brazil Petrobras mara baada ya kumaliza mazungumzo ya mashirikano kati ya pande hizo mbili. Mazungumzo hayo yalifanyika leo makao makuu ya kampuni hiyo jijini Rio de Janeiro.
  • Kampuni ya Petrobras imeonesha nia yake ya kushirikiana na Balozi Abdulsamad kupitia Jumuia ya watoa huduma ya mafuta na gesi (ATOGS) katika kutoa nafasi za kuwajengea uwezo pamoja na kuangalia fursa za masoko ya bidhaa zao na kibiashara.
  • Katika mazungumzo hayo Balozi Abdulsamad alitoa rai kampuni hiyo kuwekeza tena Tanzania na kuiomba kampuni hiyo kuangalia fursa ziliopo Tanzania ikiwemo: Domestic Production and Marketing of Liquefied Natural Gas (LPG); Domestic Manufacturing of LPG cylinders, Retail distribution less expensive gas burners kutokomeza utumiaji wa makaa; Uanzishwaji wa processing plants pamoja na industries for the production of; refined mineral oil, petroleum jelly and grease; Uanzishwaji wa chemical industries; Maendeleo ya viwanda vya petrochemicals; Uanzishwaji of LNG Projects na Crude oil refining with efficient export facilities.
BZ 3-01
Mazungumzo ya mashirikano kati ya pande mbili yakiendelea,Mazungumzo hayo yalifanyika jijini Rio de Janeiro.
  • Wakati huo huo Balozi Abdulsamad amewaalika kampuni ya Petrobras kuja Tanzania kwenye Kongamano la Mafuta na Gesi tatehe 2-3 October 2019 ili kutoa uzoefu yao kwenye sekta hiyo ya mafuta na gesi.
BZ 4-01
Ujumbe wa Wafanya biashara pamoja na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mashirika ya serikali kutoka Tanzania ikiongozwa na mkuu wa msafara Balozi Abdulsamad Abdulrahim ambae pia ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Mafuta na Gesi nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais na watendaji wakuu wa kampuni ya mafuta na gesi ya Brazil Petrobras mara baada ya kumaliza mazungumzo ya mashirikano kati ya pande hizo mbili. Mazungumzo hayo yalifanyika leo makao makuu ya kampuni hiyo jijini Rio de Janeiro.
  • Baada kikao cha Petrobras, ujumbe huo ulionana na kampuni ya Brazilian Petroleum, Gas and Biofuels Institute (IBP) Iliyoanzishwa zaidi ya miaka 62 iliyopita na ina uzoefu mkubwa katika masuala ya udhibiti, viwango, masoko, uendelezaji masoko, utafiti na uendelezaji wa wataalamu wa sekta ya mafuta na gesi nchini Brazil. IBP imelifurahishwa sana kuona juhudi zinazochukuliwa na Balozi Abdulsamad kuwasaida raia wa Tanzania kuhakikisha wanapewa ujuzi, fursa na kujengewa uwezo.
BZ
Ujumbe wa Wafanya biashara pamoja na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mashirika ya serikali kutoka Tanzania ikiongozwa na mkuu wa msafara Balozi Abdulsamad Abdulrahim ambae pia ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Mafuta na Gesi nchini, pamoja na Makamu wa Rais na watendaji wakuu wa kampuni ya mafuta na gesi ya Brazil Petrobras wakifatilia Mazungumzo hayo yalifanyika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Rio de Janeiro.
  • Kampuni ya IPB imeonesha utayari wake wa kusaini mkataba wa Makubaliano (MoU) baina ya Kampuni hiyo na Jumuia ya Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi nchini (ATOGS) katika nyanja ya kuwajengea uwezo, ujuzi wa kiufundi, udhamini wa masomo ya mafuta na gesi, pamoja na kushirikiana na kukuza kipaji cha raia wa Tanzania katika utafutaji na kutoa huduma katika sekta hiyo,(MoU) itatatiwa saini baada ya  matayarisho kukamilika hivi karibuni.
Ad

Unaweza kuangalia pia

“Tusikubali Kuwa Tarumbeta za Watu Wasio Tutakia Mema”

“Tusikubali kuwa tarumbeta za Watu wasio tutakia mema, Maadili Yetu Mazuri Ya Kitanzania Lazima Tuyatunze, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *