RAIS DKT.SHEIN AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA SIKU YA UTUMISHI WA UMMA

  • Uongozi wa Ofisi ya Rais na Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana na Chuo cha Utawala wa Umma (IPA) umetakiwa kuandaa programu maalum ya mafunzo ya muda mfupi kwa ajili ya Viongozi, Watendaji Wakuu na Watumishi wengine wa Serikali.
Z
Waziri wa Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haruna, kizungumza katika ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma Zanzibar yaliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul wakil, Kikwajuni mjini Zanzibar.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein aliyasema hayo leo katika ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma Zanzibar yaliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul wakil, Kikwajuni mjini Zanzibar.
  • Katika hotuba yake hiyo, Rais Dk. Shein alisema kuwa programu hiyo ya mafunzo ya muda mfupi kwa ajili ya viongozi hao yana lengo la kuongeza ufanisi katika Utumishi wa Umma ili wapate masomo ya kuwakumbusha majukumu yao na kuweza kuwahudumikia vyema wananchi.
ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza katika ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma Zanzibar yaliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul wakil, Kikwajuni mjini Zanzibar.
  • Rais Dk. Shein katika hotuba yake hiyo alieleza kuwa ubunifu ni muhimu katika utumishi wa Umma na ndio utakaowafanya watumishi kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
  • Alisisitiza kwamba bila ya kuwa wabunifu Zanzibar inaweza kubaki nyuma katika karne hii ya sayansi na teknolojia ambapo kwa bahati mbaya miongoni mwa watumishi wapo wachache ambao ni wagumu kubadilika katika kutimiza majukumu yao ya utumishi.
Z 4-01
Wageni wakifatilia ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma Zanzibar yaliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul wakil, Kikwajuni mjini Zanzibar.
  • Aliongeza kuwa watumishi wa aina hiyo ni lazima wabadilike na wahakikishe wanakwenda na kasi ya kutoa huduma zilizo bora na kutoa nasaha zake za kuhakikisha watumishi wanakuwa wabunifu wa kutafuta njia bora, rahisi na nzuri ya kuwatumikia wananchi ambao ndio waajiri.
  • Rais Dk. Shein alisema haja ya kuwepo kwa Chuo cha Utumishi wa Umma ambacho kutokana na mahitaji maalumu ya kitaalamu, maadili, fikra, mawazo na tabia zinazohitajika kwa wafanyakazi katika sekta ya umma nchi zote duniani zina vyuo maalum vya kutoa mafunzo maalum kwa watumishi wa umma.
  • Alieleza kuwa utumishi wa Umma ulio bora ni chachu muhimu katika kuongeza kasi ya maendeleo hapa nchini kiuchumi na kuuimarisha ustawi wa jamii hasa kwa kutambua kuwa utumishi wa Umma ni kigezo muhimu cha misingi ya Utawala Bora.
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE:RAIS MAGUFULI KATIKA UTIAJI SAINI MAKUBALIANO KATI YA SERIKALI NA KAMPUNI YA MADINI YA BARRICK

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *