RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA AMALIZA ZIARA YAKE NCHINI

  • Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta leo tarehe 06 Julai, 2019 amerejea nchini Kenya baada ya kumaliza ziara yake binafsi ya siku 2 aliyomtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Wilaya ya Chato Mkoani Geita.
KJ 2-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta katika uwanja wa ndege wa Chato mara baada ya kumaliza ziara yake binafsi ya siku mbili Chato mkoani Geita.
  • Kabla ya kuruka katika uwanja wa ndege wa Chato, Mhe. Rais Kenyatta amefanya mazungumzo ya faragha na mwenyeji wake, Mhe. Rais Magufuli katika Kijiji cha Mlimani na baada ya mazungumzo hayo viongozi hao wamezungumza na waandishi wa habari.
KJ-1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta katika uwanja wa ndege wa Chato mara baada ya kumaliza ziara yake binafsi ya siku mbili Chato mkoani Geita.
  • Viongozi hao wamesema mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na Kenya hususani katika masuala ya kiuchumi ambapo wametaka biashara baina ya nchi hizo ikuzwe zaidi pamoja na kujenga uwiano wa kibiashara wenye maslahi kwa pande zote.
KJ 9-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kabla ya kuondoka katika kijiji cha Mlimani Chato na kurejea nchini kwake Kenya.
  • Mhe. Rais Magufuli amesema kwa kuzingatia kuwa Kenya imefanya uwekezaji mkubwa zaidi nchini Tanzania ikilinganishwa na uwekezaji wa Tanzania nchini Kenya, wamekubaliana kuwa kampuni za Kenya zijielekeza kuongeza thamani ya bidhaa kwa kuanzisha viwanda vitakavyosindika mazao na kuchakata bidhaa mbalimbali hapahapa Tanzania badala ya kusafirisha malighafi kwenda Kenya.
KJ 6-01
Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta akizungumza na wanahabari mara baada ya mazungumzo yake na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
  • Ameongeza kuwa wamekubaliana kuwa Kenya itanunua gesi ya Tanzania badala ya kuagiza kutoka nje ya Bara la Afrika kwa kuwa Tanzania imejaaliwa gesi nyingi, na wamewaagiza Mawaziri wa Tanzania na Kenya kukutana na kujadili namna Kenya itavyonunua gesi hiyo.
KJ 8-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kabla ya kuanza mazungumzo yao Chato mkoani Geita.
  • Kuhusu ziwa Victoria ambalo kwa asilimia 51 lipo Tanzania na kwa asilimia 5 lipo Kenya, Mhe. Rais Magufuli amesema wamekubaliana kuwa Mawaziri wa nchi hizo wahakikishe meli za Tanzania na Kenya zinaimarishwa na kuondoa vikwazo vinavyokwamisha meli hizo kufanya kazi ya kukuza biashara katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda ambazo zinazunguka ziwa hilo.
KJ-7-01.png
Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta akiweka shada la maua katika moja ya makaburi ya Familia ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli yaliyopo katika kijiji cha Mlimani Chato wakati akiwa katika ziara yake binafsi ya siku mbili.
  • Kwa upande wake, Mhe. Rais Uhuru Kenyatta amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa mapokezi mazuri aliyoyapata hapa Chato, na kwa upendo mkubwa uliooneshwa na wananchi wa Chato kwake na ujumbe wake, na ameeleza kuwa huo ni uthibitisho wa uhusiano mzuri, undugu na urafiki wa karibu wa Wakenya na Watanzania.
KJ 4-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta wakati wakisikiliza nyimbo iliyokuwa ikiimbwa na wanakwaya wa Mwagazege ya Chato kabla ya Rais Kenyatta kuondoka na kurejea nchini Kenya.
  • Amesema pamoja na kuimarisha zaidi uhusiano wa Tanzania na Kenya uliojengwa na Waasisi wa Mataifa hayo Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mzee Jomo Kenyatta, wamekubaliana kuhakikisha nchi hizo zinakuwa na amani na kuheshimu mkataba wa kukabiliana na uhalifu ambapo Mtanzania atakayekamatwa kwa uhalifu nchini Kenya anashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za Kenya na Mkenya atakayekamatwa kwa uhalifu nchini Tanzania anashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania.
KJ 5-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta wakati wakisikiliza nyimbo iliyokuwa ikiimbwa na wanakwaya wa Mwagazege ya Chato kabla ya Rais Kenyatta kuondoka na kurejea nchini Kenya.
  • Mhe. Uhuru Kenyatta amesisitiza kuwa Wakenya na Watanzania hawana sababu ya kupoteza muda kwa mambo yasiyo ya msingi bali kuhakikisha uchumi unakua, biashara inaongezeka na uhusiano na ushirikiano katika maeneo mbalimbali unaimarika zaidi.
KJ 3-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta wakati wakipita kwenye Gadi ya Heshma iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ katika uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita.
  • Aidha, Mhe. Rais Magufuli na Mhe. Rais Kenyatta wamekubaliana kuwakutanisha wake wa waasisi wa Mataifa ya Tanzania, Kenya na Uganda ambao ni Mama Maria Nyerere, Mama Ngina Kenyatta na Mama Miria Obote kwa siku 3 Jijini Dar es Salaam ili wapate muda wa kujadiliana pamoja na kukumbuka misingi iliyowekwa na waasisi wa Mataifa hayo.
KJ 10-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpungia mkono mgeni wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati akipanda ndege kurejea nchini Kenya. PICHA NA IKULU
  • Akiwa nyumbani kwa Mhe. Rais Magufuli katika Kijiji cha Mlimani Wilayani Chato Mhe. Kenyatta ameweka shada la maua katika makaburi ya familia ya Mhe. Rais Magufuli na pia amemtembelea tena Mama Mzazi wa Mhe. Rais Magufuli, Bibi Suzana Magufuli ambaye baada ya kupatiwa matibabu ya kiharusi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam anaendelea kupata matibabu hayo akiwa nyumbani.
12
Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta akimsalimia Mama mzazi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Bibi Suzana Magufuli ambaye anapatiwa matibabu kijijini kwake Mlimani Chato mkoani Geita kabla ya kuondoka kurejea Kenya mara baada ya kumaliza ziara yake binafsi ya siku mbili.
  • Pamoja na kumshukuru kwa kumtembelea nyumbani kwake Chato, Mhe. Rais Magufuli ametoa zawadi ya ndege wanne aina ya Tausi kwa Mhe. Rais Kenyatta ili akawafuge na kuweka kumbukumbu nyingine ya uhusiano mzuri wa Tanzania na Kenya.
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *