SERIKALI KUOKOA TAKRIBANI BILIONI 25 KWA MWAKA ZA KUZALISHA UMEME KIGOMA.

 • Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema Serikali inatarajia kuokoa takribani shilingi bilioni 25 zinazotumika kununua mafuta mazito ya kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme katika Mkoa wa Kigoma kwa mwaka.
 • Akizungumza baada ya kutembelea kituo cha kuzalisha umeme mkoani Kigoma , Julai 12, Mgalu alisema serikali itaokoa fedha hizo, baada ya kuunganisha mkoa huo katika gridi ya taifa na kuacha kutumia umeme unaozalishwa kwa kutumia mafuta mazito.
 • Alisema kuwa tayari ujenzi njia ya kusafirisha umeme kuunganisha  Mkoa wa Kigoma katika gridi taifa umeanza ambapo itapita  katika Wilaya ya Urambo mkoani  Tabora,Nguruka, na Kidawe mkoani Kigoma.
MG 3-01
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,( katikati) akiwapa maelekezo wasimamizi wa mitambo ya kufua umeme katika kituo cha kuzalisha a umeme mkoani Kigoma.
 • Vilevile aliweka wazi kuwa tayari ujenzi wa vituo vya kupokea na kupoza umeme katika njia hiyo ya kusafirisha umeme umeanza.
 •  “Serikali imekuwa ikitumia shilingi bilioni 25, kila mwaka kununua mafuta mazito ya kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme Kigoma, lakini imekuwa ikiuuza umeme huo kwa shilingi bilioni 10 tu, hii ni hasara, hivyo tunatekeleza mpango mathubiti wa kumaliza changamoto hii”,alisema Mgalu.
 • Mradi huo ni wa kusafirisha umeme wa Kilovolti 132, na unatarajiwa kukamilika mwezi June 2020.
MG 2-01
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,( katikati) akikagua mitambo ya kuzalisha umeme katika kituo cha kufua umeme mkoani Kigoma
 • Akizungumzia hali ya upatikanaji wa umeme katika mkoa huo,Mgalu alisema mkoa huo unahitaji umeme zaidi, ila kwa sasa upo mpango wa kuongeza mitambo ya kufua umeme katika wilaya zenye mahitaji  makubwa zaidi ikiwemo Wilaya ya Kasulu.
 • Mitambo hiyo ni ile iliyozimwa katika mikoa ambayo ilikuwa inatumia mafuta mazito kufua umeme , ambapo kwa sasa tayari imeunganishwa katika gridi ya taifa, na kuacha kutumia umeme unaozalishwa kwa  kutumia mafuta mazito.
 • Sambasamba na hilo, alitoa wito kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)kuwa, ujenzi wa njia ya umeme ukikamilika uende sambasamba na uimarishaji wa upatikanaji wa huduma ya umeme.
MG 1-01
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akisaini kitabu cha wageni katika kituo cha kuzalisha umeme, alipofanya ziara ya kukagua utendaji kazi katika kituo hicho.
 • Pia kusitokee changamo ya kukatika kwa umeme mara kwa mara kwa lengo la kuwapatia huduma bora watumiaji katika kuendesha shughuli  za uzalishaji.
 • “ Tanesco katika mradi huu mjipange,mtimize azma ya serikali ya kuwapatia wananchi umeme wa kutosha na wa uhakika,wananchi wajue kweli wameingia kwenye gridi, siyo wanaingia kwenye gridi umeme unakatika hapana,nawapa tahadhari mapema,” alisisitiza Mgalu.
 • Akiuzungumzia fursa za Mkoa wa Kigoma, Mgalu amesema, serikali imedhamiria kuufanya Mkoa wa Kigoma kuwa  wenye viwanda na kuwavutia zaidi wawekezaji kwa kuwa mazingira yanaruhusu. Na Zuena Msuya Kigoma
Ad

Unaweza kuangalia pia

TPDC YAOKOA TRILIONI 12.7 KUAGIZA MAFUTA NJE YA NCHI

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *