TUTAENDELEA KUTOA ELIMU BURE KWA WANANCHI KAMA ILIVYO KWA SEKTA YA AFYA – RAIS DKT. SHEIN

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa elimu bure kwa wananchi wake kama ilivyo kwa sekta ya afya na katu haitorudi nyuma.
  • Rais Dk. Shein aliyasema hayo leo katika hotuba yake aliyoitoa katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Skuli ya Sekondari Ziwakije Wingwi Mkoa wa Kaskazini Pemba ikiwa ni shamrashamra za sherehe za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Katika hotuba yake hiyo, Rais Dk. Shein alisema kuwa elimu itaendelea kutolewa bure na kueleza kuwa yeyote ambaye atabadilisha malengo ya Serikali ya kutoa elimu na afya bure atachukuliwa hatua zinazofaa kwani hayo ni matunda ya Mapindyzi matukufu ya Januari 12, 1964.

2222-01

  • Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa historia ya Mapinduzi na harakati zake za kupigania huru wa wanyonge na kusema kuwa Mapinduzi yamekuja kutokana na madhila makubwa yaliokuwa wakifanyiwa Waafrika wa Zanzibar.
  • Aleleza kwua Watawala wa Kwanza walikuwa Wareno ambao walikuja mnamo mwaka 1503 ambao walikaa zaidi ya karne tatu ambapo baadae waliondoshwa na ndipo alipokuja Mfalme wa Oman na kufanya maskani Zanzibar na kujitangaza kuitawala Zanzibar.
  • Alisema kuwa zaidi ya miaka 300 Zanzibar ilitawaliwa na Wakoloni ambapo kabla ya hapo Zanzibar ilikuwa huru na kusema kwamba mpaka yanafanyika Mapinduzi mwaka 1964 wanyonge walikuwa hawapati nafasi ya kusoma.

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

KAMPUNI YA SIGARA TANZANIA(TCC) KUTOA MSAADA WA VIFAA MBALIMBALI KWA WATU WENYE ULEMAVU ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba utayari wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *