HUDUMA YA KUVUNJA MAWE KWENYE FIGO KWA TEKNOLOJIA YA KISASA YAANZA MLOGANZILA

Hospitali ya Taifa Muhimbili -Mloganzila imeanza rasmi huduma ya kuvunja mawe kwenye figo na mfumo wa mkojo kwa kutumia njia ya mawimbi mshituko kwa kitaalamu extracorporeal shock wave lithotripsy (ESWL) .

Kuanzishwa kwa matibabu haya ni mwendelezo wa kutekeleza juhudi za Serikali kuboresha huduma bobezi za kibingwa nchini ili kuongeza wigo wa huduma ambazo hapo awali zilikua hazipatikani hapa nchini kutokana na kutokuwepo kwa watalaam, vifaa tiba au vyote viwili. Huduma hii inatolewa na watalaam wazawa walioko Upanga na Mloganzila.

Ad


Huduma hii inafanywa kwa kutumia mashine ambayo inatoa mawimbi sauti yanayosafiri kupitia ngozi hadi kwenye figo sehemu yenye jiwe au mawe. Mawimbi hayo hugeuka kuwa nishati yenye uwezo wa kuvunja mawe kuwa madogo mithili ya mchanga ambapo yakishasagwa yatatoka kwa njia ya haja ndogo (kukojoa).

Tumeanza kutoa huduma hii mapema mwezi Juni mwaka huu, kama tulivyowaahidi wa Tanzania ambapo jumla ya wagonjwa nane wamenufaika na matibabu haya ambayo yameonesha matokeo mazuri. Leo, wagonjwa wawili wanaendelea kuhudumiwa hivyo kufikisha idadi ya wagonjwa 10 tangu ilipoanzishwa.

Gharama ya kutoa matibabu haya kwa mgonjwa mmoja ni kati ya TZS. 500,000 hadi TZS. 1. 2 Mil kulingana na kundi alilopo mgonjwa (rufaa au binafsi) na raia wa kigeni itakua TZS. 4.8 Mil, endapo akipelekwa nje ya nchi itagharimu TSZ. 10 Mil kwa mgonjwa mmoja. Hivyo kufuatia matibabu haya waliopatiwa wagonjwa 10, serikali imefanikiwa kuokoa kiasi cha TZS 95 Mil.


Katika kipindi cha mwaka 2019, jumla ya wagonjwa 1035 wenye mawe kwenye figo walionwa katika kliniki za wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga na Mloganzila, kati ya hao wagonjwa wapya walikuwa 425 wakati wagonjwa waliolazwa kutokana na tatizo hilo walikuwa 114, na 50 wastani wagonjwa wanne kwa mwezi walifanyiwa upasuaji kuondoa haya mawe.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA ATEMBELEA RUKWA.. AANGAZIA AFYA, ELIMU, KILIMO NA MIUNDOMBINU KWA MIRADI YA MAENDELEO.

Katika ziara ya Rais Samia siku ya leo iliangazia kwenye sekta ya Afya, Elimu, Kilimo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *