MAKAMU WA RAIS SAMIA AMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE KUAPISHWA RAIS MPYA WA BURUNDI

Makamu wa Rais wa Jarmhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete wakiwa na Rais Mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye mara baada ya Rais Ndayishimiye kuapishwa kuwa  Rais wa Jamhuri ya Watu wa Burundi Juni 18,2020 katika Uwanja wa Ingoma Stadium Nchini Burundi Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais Mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Burundi Juni 18,2020 katika Uwanja wa Ingoma Stadium Nchini Burundi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa  na Rais mpya wa Burundi Evariste Ndayishimiye wakati Rais Ndayishimiye alipokuwa akipokea Gwaride la Jeshi la Wananchi wa Burundi baada ya kuapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Burundi Juni 18,2020 katika Uwanja wa Igoma Stadium Nchini Burundi. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Shughuli hiyo.
Rais  Mpya Burundi Evariste Ndayishimiye  akikaguwa Gwaride baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Burundi Juni 18,2020 katika Uwanja wa Ingoma Nchini Burundi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais  Mpya wa  Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye Ikulu ndogo Gitega Nchini Burundi  alipowasilisha salam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Rais Ndayishimiye Juni 18,2020.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais  Mpya wa  Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye Ikulu ndogo Gitega Nchini Burundi  alipowasilisha salam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Rais Ndayishimiye Juni 18,2020. kushoto ni Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete.
Ad

Unaweza kuangalia pia

Je! Wajua Mchango wa Madini ya Tanzanite katika Pato la Taifa?

Madini ya Tanzanite, yanayopatikana pekee katika eneo dogo la Mererani, Tanzania, ni miongoni mwa rasilimali …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *