TANESCO WAPEWA SIKU TANO KULIPA FIDIA KWA WANANCHI WA KIDAHWE

Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kidahwe,kata ya Kidahwe Wilaya ya Kigoma vijiji, Mkoani Kigoma,wakati akiwa kwenye uzinduzi wa kuanza malipo kwa wananchi ambao wameridhia kutoa ardhi yao kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Kupoza umeme cha Kidahwe.

Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani ametoa siku tano kwa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) kulipa fidia kwa wananchi  wa Kidahwe waliopisha ujenzi wa kituo cha kupoza  umeme(substation) cha Kidahwe kilichopo katika kijiji cha Kidahwe,kata ya Kidahwe wilaya ya Kigoma vijijini, Mkoani Kigoma.

Agizo hilo amelitoa 27 Juni 2020, wakati akiwa kwenye uzinduzi wa kuanza malipo kwa wananchi ambao wameridhia kutoa ardhi yao kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Kupoza umeme cha Kidahwe.

Ad
Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika kukagua ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Nguruka, Kilichopa katika kijiji cha Mganza Wilaya ya Uvinza,Mkoani Kigoma.

Akizungumza kwenye tukio hilo alisema, zaidi ya shilingi milioni mia saba zipo tayari kwaajili ya malipo ya wananchi 411 na kuwataka TANESCO kuanza mara moja kuwalipa wananchi hao na kuwapa siku tano tu kumaliza zoezi hilo.

“Niliacha maelekezo kwa waatalamu wetu kufanya kazi mbili, kazi ya kwanza ilikuwa kuhakikisha wananchi wanaozunguka maeneo ya mradi ambao wanapitiwa  mradi wafanyiwe tathimini na kulipwa fidia zao na jambo hili tayari limeanza kufanyiwa kazi na jambo la pili ni kuanza matayarisho ya ujenzi wa mradi mkubwa huu,”Alisema Dkt Kalemani.

Aidha, Dkt Kalemani aliwashukuru wananchi wa eneo hilo kwa kutoa maeneo yao kwaajili ya ujenzi wa kituo hicho kikubwa  chenye uwezo wa kuzalisha umeme wa Kv 400, umeme huo ambao  unatarajiwa kuondoa kero ya upatikanaji wa umeme Mkoani humo.

Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani(mwenye miwani) akitoka kukagua ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Nguruka, Kilichopa katika kijiji cha Mganza Wilaya ya Uvinza,Mkoani Kigoma.

Hafsa Omar – Kigoma

Dkt Kalemani amewataka wananchi watakaolipwa fidia hiyo kuzitumia vizuri fedha zao vizuri  kwa kununua maeneo mengine na kujiendeleza kiuchumi.

“Mtakao lipwa fedha zenu msije mkazitumia vibaya hiyo hela halafu mkarudi tena TANESCO kudai hela nyengine hakuna hela nyingine hela ni hiyo hiyo utakayolipwa” Alisema.

Vilevile,aliwataka TANESCO kuanzia tarehe 5 Julai waanze mara moja ujenzi wa kituo hicho, ili wananchi wa Kigoma waanze kupata umeme wa uhakika ambao utawasaidi kujenga uchumi wa Mkoa huo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Emmanuel Maganga amewashukuru wananchi wote waliotoa maeneo yao kwaajili ya maendeleo ya Mkoa huo na amewahakikisha pesa zipo tayari kwaajili ya malipo yao.

Pia,aliwatahadharisha wale wote watakaolipwa fidia hawataruhusia kuyatumia tena maeneo hayo kwani maeneo hayo yatakuwa ni mali ya Serikali kwasababu watakuwa tayari Serikali imeyalipia.

Katika ziara yake hiyo mkoani Kigoma, Dkt Kalemani pia ametembea kwenye kituo cha kupoza umeme cha Nguruka kilichopo katika kijiji cha Mganza na kuwataka TANESCO kumaliza ujenzi wa kituo hicho Julai mwaka huu.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Na Haya Ni Maboresho Makubwa katika Sekta ya Afya Nchini Tanzania

Nchi yetu inajivunia hatua kubwa tunazoendelea kupiga kwenye eneo hili ambapo pamoja na maboresho na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *