MIGODI LAZIMA ITEKELEZE SHERIA YA “LOCAL CONTENT” – WAZIRI BITEKO

Na. Issa Mtuwa – WM – Geita

Waziri wa Madini amesema yapo mambo mengi yanayozungumzwa na kukubaliana kati ya Serikali na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) hususani ulipaji wa Kodi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya jamii (CSR) lakini bado baadhi hakubaliani nayo hususani suala la utekelezaji wa masuala ya utoaaji huduma za Kibiashara (Local Content) kwani nafasi hiyo ndio inayowapa wazawa kushiriki shuguli za uchumi kupitia sekta ya Madini.

Ad

Hayo yamesemwa jana mkoani Geita na Waziri wa Madini Doto Biteko alipotembelea mgodi mkubwa wa Dhahabu wa Geita (GGML) kukagua shuguli zinazofanywa mgodini hapo.

Amesema, fursa za watu kushiriki katika utoaji huduma za kibiashara mgodini, ni muhimu kuwapa fursa wazawa ili kuinuwa uchumi wao na taifa. Aliongeza kuwa kazi zinazoweza kufanyika mgodini lazima zifanywe na Watanzania na kwamba kitendo cha hoja ya GGML kutaka kutoa huduma za kufanya tathmini    za uingizaji umeme mgodini hapo, haweze kuidhinisha, vinginevyo Wizara ya Nishati iseme hakuna mtaalam hapa nchini wa kufanya kazi hiyo.

Waziri wa Madini Doto Biteko akiwaonesha Waandishi wa Habari baadhi ya mambo yaliyowasilishwa kwake na Makamu wa Rais wa Mgodi wa GGM Simon Shayo.

Biteko amezungumzia pia, kuhusu haki ya wananchi hasa kwenye migogoro ya fidia.  Ameongeza kuwa hayupo tayari kuona hata mtu mmoja anadhulumiwa haki yake inayopitia sekta ya madini.

“Manyanyaso ya wanyonge yanayotokana na sekta ya madini, yananiumiza sana, inaniuma kwa sababu, hata alienipa mamlaka haya, aliniambie nije kutatua kero za wananchi kwenye sekta ya madini” alisema Biteko.

Amebainisha kuwa, kijiji cha Magema wananyanyasika kuhusu mahali wanapoishi, huku mgodi ukihitaji eneo hilo. Toka walipoomba walipwe fidia mpaka leo jambo hilo halijatekelezwa.

Waziri wa Madini Doto Biteko katikati akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel kulia, na Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idrisa Kikula kushoto.

Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, amesema ameteuwa Kamati ya wataalam mbalimbali kufuatilia na kuweka mpango mkakati utakao wahusisha wananchi katika kuto huduma za kibiashara mgoni hapo kutoka asilimia 31 hadi asimilia 80, huku akiwa tayari kwenda Magema kufanya tathmini ya uhakiki nani mwenye haki na nani asie na haki ili utekelezaji wa fidia ufanyike.

Makamu wa Rais wa Mgodi wa GGML Simon Shayo amesema mgodi wao upo siku zote kushirikiana na kutekeleza maelekezo ya serikali. Kuhusu utekelezaji wa maagizo ya serikali kuhusu suala la umeme, Local Content na tathmini ya fidia yatazingatiwa.

Shayo ameongeza kuwa, kuhusu ajira na Local Content, mgodi huo unatekeleza vizuri sana huku jumla ya wafanyakazi zaidi ya 4000 wameajiriwa mgodini hapo huku upatikanaji wa huduma za kibiashara za Watanzania imefikia asilimia 31.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Uzinduzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya UCSAF Dodoma: Kuimarisha Mawasiliano Vijijini

25 Aprili 2024, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *