AGIZO LA RAIS DKT MAGUFULI LAANZA KUTEKELEZWA MKOANI MOROGORO

Wananchi wa eneo la Ilonga Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wamemshukuru Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kutekeleza ahadi yake  ya kuunda kamati maalum ya kutatua kero za migogoro ya ardhi inayosababisha maafa kwa wananchi pamoja na ukosefu wa huduma za afya baada ya mmojawapo wa wajumbe wa kamati hiyo kufika katika eneo hilo kwa lengo la kuanza kuzitatua kero hizo. 

Mjumbe wa Kamati maalum iliyoundwa kwa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli,ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi amefika katika eneo la la Ilonga kukagua eneo ambalo kunatarajiwa kujengwa kituo kikubwa cha afya chenye uwezo wa kufanya upasuaji 

Ad
Waziri wa Mambo Nje Prof. Palamgamba Kabudi

Prof. Palamgamba amesema kuwa amelazimika kufika na kujionea eneo ambapo kunatarajiwa kujengwa kituo hicho na kuagiza kutafutwa eneo jingine lenye ukubwa wa heka 15 badala ya 10 za awali ili kituo cha afya kitakachojengwa kikidhi haja ya kuhudumia maeneo mengine mbali ambapo kwa Ilonga pekee kituo hicho kinatarajiwa kuhudumia wananchi zadi ya 2000.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi amesema kamati maalum iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia Dkt. John Pombe Magufuli tayari imeanza utekelezaji wa awali ambapo Makatibu wakuu wa Wizara mbalimbali wamefika Wilayani Kilosa na kwamba ujio wa Prof. Kabudi unaashiria kuanza mara moja utekelezaji wa maagizo hayo.

Nao baadhi ya wananchi mbali na kero hiyo ya huduma ya afya wameomba kusogezewa karibu huduma ya maji safi na salama kutokana na kutokuwepo kwa huduma hiyo jambo ambalo linahatarisha Maisha ya watoto na akina mama wanakwenda umbali mrefu kutafuta huduma ya maji safi na salama.

Prof. Kabudi kesho anatarajiwa pia kujionea na kukagua maeneo ya mashamba makubwa yenye mgogoro baina ya wananchi na wawekezaji ikiwa ni mojawapo ya njia ya kutafuta suluhu ya kudumu baada ya agizo la Rais.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mama Mzazi wa Mama Janeth Magufuli (Juliana Stephano Kidaso) katika eneo la Kigongo Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *