UFUNGAJI WA SCANNER KUBWA YA KISASA AFRIKA INAYOTUMIA MIONZI KUKAGUA MIZIGO INAYOPITA BANDARI YA DSM, WARIDHISHA

Jengo la kuendeshea mitambo na udhibiti midaki (Scanner) kubwa na ya kisasa Afrika ya kukagua mizigo inayopita katika Bandari ya Dar Es Salaam, lilivyoonekana wakati wa ziara Wajumbe wa Kamati ya usimamizi wa Mradi wa uboreshaji wa Taasisi za usimamizi wa Rasilimali Asilia na Ukusanyaji wa Mapato (PSC) unayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na Serikali,waliyoifanya ya kukagua ujenzi na ufungaji wa midaki hiyo Julai 9,2020.

Kamati ya usimamizi wa Mradi wa uboreshaji wa Taasisi za usimamizi wa Rasilimali Asilia na Ukusanyaji wa Mapato (PSC)unayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na Serikali imeridhishwa na kasi ya ufungaji wa Midaki (Scanner) kubwa na ya kisasa Afrika katika bandari ya Dar Es Salaam inayotumia mionzi kukagua mizigo.

Mradi huo upo chini ya Wizara ya Nishati ambao unasimamiwa na kutekelezwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuanzia ngazi ya manunuzi: Ujenzi wa jengo la Midaki hiyo umekamilika kwa 99%, kazi ya usimikaji na ufungaji wa vifaa imekamilika kwa 51%, ambapo inatarajiwa kukamilika mwezi Septemba 2020, kwa gharama ya zaidi ya Dola za kimarekani milioni 5, zikiwemo na fedha za kitanzania.

Ad
Jengo la midaki (Scanner) kubwa na ya kisasa Afrika ya kukagua mizigo inayopita katika bandari ya Dar Es Salaam, lililokamilika kwa zaidi ya 90% lilivyoonekana wakati wa ziara Wajumbe wa Kamati ya usimamizi wa Mradi wa uboreshaji wa Taasisi za usimamizi wa Rasilimali Asilia na Ukusanyaji wa Mapato (PSC) unayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na Serikali,waliyoifanya ya kukagua ujenzi na ufungaji wa midaki hiyo Julai 9,2020

Hayo yameelezwa na Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo,Kamishna wa Petroli na Gesi wa Wizara ya Nishati,Adam Zuber, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo,ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said, walipofanya zaira ya kukagua maendeleo ya ufungaji wa midaki hiyo katika bandari ya Dar es salaam, Julai 7,2020.

Zuber alisema kuwa midaki hiyo itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kukagua magari makubwa ya mizigo mia mbili kwa saa, hivyo karahisisha utendaji kazi katika bandari hiyo na kuwatoa huduma kwa haraka kwa wateja.

Wajumbe wa Kamati ya usimamizi wa Mradi wa uboreshaji wa Taasisi za usimamizi wa Rasilimali Asilia na Ukusanyaji wa Mapato (PSC)unayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na Serikali,wakiwa katika kikao cha mwisho wa mwaka wa fedha 2019/2020 kabla ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi na ufungaji wa midaki (Scanner) kubwa na ya kisasa Afrika ya kukagua mizigo inaypita katika bandari ya Dar Es Salaam, Julai 9,2020.

Na Zuena Msuya, Dar Es Salaam,

Midaki hii itakuwa na uwezo wa kubaini aina mbalimbali za mizigo inayongia na kutoka nje ya nchi kupitia bandari hiyo, kuondoa udanganyifu uliokuwa unafanya na baadhi ya wafanyabiashara wasiowaaminifu waliokuwa wakipitisha bidhaa tofauti na zile zilizoelezwa katika nyaraka husika.

Alisema kuwa midaki hiyo pia,itaongeza kwa kiasi kikubwa kasi ya ukusanyaji mapato ya serikali kwa kuwa itakuwa na uwezo mkubwa wa kubaini na kukagua kila kitu kilichomo katika shehena ya mzigo ili ilipiwe kodi stahiki.

“Hii Midaki(scanner) ni muhimu sana kwa taifa letu, itarahisisha ukusanyaji wa mapato, kubaini kilichobebwa ndani ya gari, na kusafirisha mizigo kwa haraka zaidi, kimsingi kamati imeridhishwa na kasi ya ujenzi wake,na tunaipongeza sana TPDC kwa kazi nzuri,hii ni midaki(Scanner) kubwa na ya kisasa kwa nchi za Afrika,”alisema Zuber.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio, aliwahakikishia watanzania kuwa anaimani midaki hiyo itakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa kwa kuwa asilimia kubwa ya utekelezaji wa mradi huo imekamilika.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Benki ya NMB Tanzania yapongezwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

kwakuwa Kinara katika utendaji wake, kutengeneza faida kubwa ya mfano wa kuigwa na mashirika na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *