MIMI NASEMA OKTOBA UTAENDELEA KUWA RAIS WA TANZANIA – JOHN CHEYO

Alichozungumza Mwenyekiti ya UDP John Cheyo Ikulu Jijini Dodom Julai 12, 2020

“Mhe. Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania na mimi nasema Oktoba utaendelea kuwa Rais wa Tanzania, nasema hili kwa kujivuna kabisa jana Mhe. Rais kidogo nilipata wivu ulikuwa unamwinua Mrema asante Mrema kwa kutuunga mkono na kumbe wa kwanza kabisa kukuunga mkono ni United Democratic Party (UDP) na sababu zangu ni chache tu”

Ad

“La kwanza najivunia kuwa Mtanzania ni wapi katika nchi zote ulimwenguni unaweza ukakubaliwa kuhutubia kongamano kubwa, mkutano mkubwa kwa heshima kama huu wa Chama cha Mapinduzi na wewe si mwanachama wa chama cha Mapinduzi hata Amerika kwa Trump hawafanyi hivyo mimi najivunia kuwa Mtanzania na yule binti aliyeimba ni raha ni raha kweli kuwa Mtanzania na washangaa sana watu ambao wanajihita wapinzani ambao wanatembea Ulaya, Amerika wakiiponda Nchi tamu kama hii ya Tanzania”

“Na chini ya uongozi Magufuli nashangaa sana, kweli nyinyi watu wa CCM mnapaswa kujivuna kuwa na Mwenyekiti kama Magufuli amewangarisha mseme kweli mpenzi wa Mungu miaka mitano iliyopita mlikuwa mmesambaratika na mngesambaratishwa lakini sasa mko wapoja hongereni sana na hongera sana Mhe. Mwenyekiti kwa kujenga Chama imara kama ambavyo kinaonekana sasa”

“Sisi UDP tumetangaza kwamba mgombea wetu urais ni Magufuli na leo (Julai 12, 2020) kwasababu labda hii radio inasilikizwa sehemu nyingine, sema kweli nawaonea huruma watakao mpinga Magufuli, ngoma ishamalizika”

“UDP sisi tunaowamba tu kidogo kwamba angalau tupate diwani hata mmoja tupate wabunge wawili, watatu na tunataka madiwani na wabunge hao kwasababu moja tu ya msingi tangu nimeanza siasa nilisema nchi hii ni tajiri na sasa ndio wimbo wa Rais wangu safi sana Mhe”

“Lakini tangu nimeanza siasa nilikuta wakulima wana shida sana walikuwa wanakopwa mazao yao kila siku naomba nipate wabunge wawili au watatu ili wakiwa bungeni wapaze sauti moja ni marufuku kumkopa mkulima na iwe sheria moja tu no cash no korosho, no cash no cotton hilo tu Mhe kama nimekuhudhi utanisamehe lakini ukiwawezesha wakulima umetengeneza, wazungu wanasema taxable society watu ambao unaweza kuchukua kodi kwasababu kwa chochote watakachopata wataenda kununua mabati na ndani yake kuna asilimia 18 inayoenda kama VAT inayoenda serikalini kwahiyo naomba ni hilo tu”

“Lakini lingine ambalo nataka kuwaomba wezangu hakuna chama kilichoandikishwa kama chama cha upinzani vyama vilivyoandikiswa ni kwa majina yake mbalimbali wala hakuna chama kilichoandikishwa kwenda kuiondoa CCM ukiweka hilo mimi nakwambia hutapata usajili wa kudumu sasa hii biashara ebu tuungane jamani 2020 ili tukaiondoe CCM uiondoe CCM uweke nini?”

“Mhe Rais mkiniendekeza mimi nitaendelea kuwashindilia afadhali niachie hapa nikuombee kila la kheri uwe na ushindi mkubwa lakini kumbuka kulipo na ushindani ndipo watu wanangarishwa hivi leo (Julai 12, 2020) kuna Simba na Yanga Dar es Salaam hapakaliki tuimarishe pia mfumo wetu wa vyama vingi mfumo hatujawa na mfumo Mwalimu hakutuachia vyama tawala na vyama vya upinzani ametuachia mfumo wa vyama vingi natamani siku moja tuweze ukatuitia kongamano utakapokuwa umeshinda pawepo na watu kutoka vyama vyote na waje wafurahi kama vile nilivyofurahi mimi leo na kina Harmonize ndio Tanzania ninayoitaka, Tanzania ya vyama vingi lakini Tanzania moja anayetuunganisha ni mama yetu Tanzania Asanteni sana “ – Mwenyekiti wa United Democratic Party (UDP) John Cheyo

Ad

Unaweza kuangalia pia

“Tusikubali Kuwa Tarumbeta za Watu Wasio Tutakia Mema”

“Tusikubali kuwa tarumbeta za Watu wasio tutakia mema, Maadili Yetu Mazuri Ya Kitanzania Lazima Tuyatunze, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *