MKATATUE MATATIZO YA WANANCHI – RAIS MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Aboubakar Kunenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 16 Julai 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Joseph Joseph Mkirikiti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 16 Julai 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi wateule kwenda kutatua matatizo ya wananchi katika maeneo yao.

Akizungumza katika hafla ya kuapisha viongozi aliwateuwa hivi karibuni leo Alhamisi (Julai 16, 2020) Ikulu, Chamwino Dodoma, Rais Magufuli aliwataka viongozi wateule kwenda kufanyakazi, kusimamia shughuli za maendelo pamoja na kutatua matatizo ya wananchi ikiwemo migogoro mbalimbali huku akitolea mfano mgogoro wa ardhi wa ulipo katika Wilaya ya Chunya, jinini Mbeya.

Ad
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Gabriel Pascal Luhende kuwa Wakili Mkuu wa Serikali katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 16 Julai 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Paulo Mshimo Makanza kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Maduhu Isaac Kazi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akimuapisha Ssgt Mayeka Simon Mayeka kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Binilith Mahenge, Katibu Mkuu TAMISEMI Eng. Joseph Nyamhanga, Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali walioapishwa leo katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Aboubakar Kunenge akila kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joseph Joseph Mkirikiti Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

“Mkatimize wajibu wenu na kufanyakazi vizuri, mkamtangulize Mungu katika shughuli zenu na mkawatumikie watanzania na hasa wananchi masikini waliopo katika maeneo yenu,” alisema Rais Magufuli

Aidha, Rais Magufuli alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt. Maduhu Isaac Kazi  ambaye ni kati ya viongozi aliowateua kuhakikisha  kuwa hakuna urasimu katika kuwawezesha  wawekezaji  kutekeleza miradi yao hapa nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akimuapisha Alhaj Rajab Kundya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi

“Tusiwazungushe wawekezaji, tuwavutie waje kuwekeza nchini, nchi yetu ina maeneo mbalimbali ya uwekezaji  ikiwemo Kigamboni na Kibaha, tuongeze kasi katika utendaji wetu ili tuendelee kujenga uchumi wetu, na sasa tumeingia uchumi wa kati basi tujitahidi zaidi” alisisitiza Rais Magufuli

Viongozi mbalimbali wakila kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma PICHA NA IKULU

Na.Immaculate Makilika – MAELEZO

Kwa upande, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliwapongeza wateule wapya na kuwataka kuwa watumishi wa watu badala ya kuhaha na madaraka waliyoyapata.

Viongozi walioapishwa ni pamoja na Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya,  Makatibu Tawala wa maeneo mbalimbali na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),ambao waliteuliwa katika nafasi hizo.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *