USICHOKE KUTULEA SISI VIJANA TUNA MIHEMKO MIKUBWA – MKUU WA MKOA WA MBEYA CHALAMILA

Alichozungumza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila Ikulu Chamwino,jijini Dodoma julai 16, 2020

“Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nifurahi kidogo kwa kupewa nafasi hii kuwa mmoja wa wazungumzaji wa kutoa neno kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa waliohudhuria hii leo”

Ad

“Mhe Rais nimepewa jina hivi karibuni kwamba ni mzee wa Uturn baada ya maneno yako ya ushauri mkubwa sana kuhusiana na sisi vijana tunaotaka kwenda kugombea nyazifa mbalimbali nilikaa nikatafakari sana Mhe Rais”

“Magezeti yakaandika nimebadilisha gear angani lakini Mhe. Rais niseme machache sana kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa wezangu, katika jiji la Mbeya ulilonipa heshima kuliongoza kuna mambo kadhaa niliyatafakari na ambayo ninafikiri hata wezangu Wakuu wa mikoa mingine hayo mambo wameyashuhudia”

“Jambo la kwanza Mhe. Rais ambalo ninalo furaha kusimama mbele yako kwanini nilipiga kona angani na kubaki nilipo baki bila ya kwenda kugombea ni haya yafuatayo jambo la kwanza Mhe. Rais katika jiji letu la Mbeya wachache wamesema hakuna maendeleo yanayotekelezwa”

“Lakini hivi karibuni Mhe Rais tumepokea shilingi Bilioni 3.9 kwaajili ya kuboresha miundo mbinu ya elimu na fedha hizi zinakwenda kugawanywa katika Halmashauri zote sasa hili ni mojawapo limenifanya nibaki jijini Mbeya ili niendelee kusimamia vizuri na kuratibu shughuli hizi za maendeleo”

“Lakini jambo la pili Mhe. Rais umeendelea kukarabati shule kongwe tumepokea milioni 8.9 katika shule ya sekondari Lolenza ambayo sasa imeshakamilika tumepokea shilingi milioni 700 kwa akili ya shule ya sekondari Rungwe na ambayo sasa ukarabati unaendelea, tumepokea shilingi milioni 700 shule ya sekondari Mbeya Day ambayo sasa pia ukarabati wake unaendelea”

“Ukarabati huu wote wa shule za sekondari Mhe. Rais umenifanya pia mimi nisiende kugombea hata kidogo ili angalau nibaki jijini Mbeya nihakikishe shule hizi na azma yako inatekelezwa vizuri tumpigie makofi Mhe. Rais”

“Lakini vilevile Mhe. Rais katika jiji letu la Mbeya umeleta fedha nyingi sana za ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya ukienda katika Wilaya ya Chunya Mhe. Rais kuna vituo vya afya vitatu kule Mamba, pale Charangwa na pale Mtande, ukienda Mbeya vijijini Mhe. Rais kuna vituo vya afya vitatu kuna pale Ikuti, kuna pale Ikukwa, Ilembo na Santiria”

“Ukienda jiji la Mbeya Mhe. Rais kuna vituo vya afya vitatu kuna kituo cha Nzovwe, Iyunga na kituo cha afya cha Igawilo ambavyo juzi umekipatia milioni 500 ukikipandisha hadhi kutoka kituo cha afya kuwa Hospital ya Wilaya”

“Ukienda kule Kyela kuna kituo cha Afya Ipinda, ukienda kule Busekelo vituo vya afya vitatu kituo cha Ntabe, Isange na vituo vingine vingi ambavyo umevitekeleza katika jiji letu la Mbeya ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Hospital kubwa tatu ulizoleta bilioni 4.5 na sasa umeendelea kuongezea milioni 300 katika Hospital mbili na milioni 500 katika Hopsitali moja”

“Hivi vituo vya afya na Hospital zote Mhe Rais pamoja na shilingi bilioni 4 ulizozileta kwaajili ya kujenga wodi kubwa ya Mama na mtoto Hospital yetu ya rufaa na ambalo sasa linakamilika na uliahidi kuleta si chini ya shilingi bilioni 6 Mhe Rais fedha hizi nilikaaa nikatafakari sana na sikuona haja hata kidogo ya kuendelea na gear yangu ya kwenda kugombea na ambapo kila nikikuangalia sijui kama ningeshinda”

“Mhe. Rais ni vichekesho lakini tunakusumbua kweli sisi tunaomba uendelee kutuwia radhi sana lakini Mhe Rais nayesema haya kwasababu gani kuna propaganda nyingi ambazo zinaendelea kwenye majiji yetu ambayo tunayaongoza sasa hivi Mhe. Rais”

“Unaendelea kukarabati uwanja wa ndege umeleta bilioni 14.7 kwaajili ya kutengeneza run way pamoja pia na fance na kutengeneza lile jengo la abiria lakini pia umeleta bilioni 4.6 kwaajili ya kuweka miundo mbinu ya taa pamoja na shuguli zingine kwahiyo sio chini ya bilioni 20 umeendelea kuzileta tayari mkandarasi ambaye anajenga One Stop center border post ya pale Kyela ndio huyo huyo anaendelea kutengeneza uwanja wetu wa ndege”

“Kwahiyo Mhe. Rais shughuli hizi ni nyingi sana tukienda kwenye mashule tunapokea kila mwezi shilingi milioni 9.1 sasa pesa hizi Mhe Rais nikiondoka nikaenda kugombea sijui kama nitakuwa nimetii na sijui kama nitakuwa na nidhamu mbele ya mamlaka”

“Niitimishe tu kwa kusema mamlaka haya na madaraka haya umetupatia wewe kwa kutuamini sana lazima na sisi tuweze kujiamini ili tukusaidie wewe kufanya kazi kubwa ya kuwaletea wananchi wetu maendeleo kwahiyo niendelee kuwa na ushauri mzuri”

“Nilimwambia Mhe. Jafo kwamba nilieeleza maneno yale nikiamini wezangu wachache watanisikiliza lakini wapi waliona kama nachekesha lakini leo wanashuhudia kwamba hakikuwa kichekesho bali ilikuwa filamu halisi Mhe. Rais baada ya kusema haya mimi nakupongeza sana na usichoke kutulea sisi vijana na mihemko mikubwa lakini mbele yako naomba nimpongeze sana Mama Mariam Tunguja Katibu Tawala wangu wa Mkoa wa Mbeya kweli amenisaidia sana kupunguza mihemko mimi kama kijana”

“Wapo watu nilipofika Mhe. Rais wakiendelea kututukana ona kijana huyu, anajidai na urefu wake wakijua mimi ni mfupi, lakini wengine wakasema ona kijana huyu amekuwa ni muhuni muhuni anayapenda mapenzi ni matusi baada ya kuwakamata wengi lakini Mhe. Rais nikudhiirishie ndio maana nilioa ili niyatumikie vizuri hayo mapenzi ambayo wanasema nayapenda lakini ukweli ni kwamba tunatukanwa kwasababu tumeshikilia sheria umeona tumekusanya mapato Mhe. Rais sasa hivi tuko vizuri tulikuwa tumekadiriwa bilioni 12 tumefikisha na mwaka huu wa fedha tumekadiriwa bilioni 15 kwa jiji tu la Mbeya tunakuhakikishia tutafikisha” – Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ALBERT CHALAMILA

Ad

Unaweza kuangalia pia

Uzinduzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya UCSAF Dodoma: Kuimarisha Mawasiliano Vijijini

25 Aprili 2024, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *