RAIS DKT. MAGUFULI AAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA HIVI KARIBUNI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhandisi Marwa Mwita Bubirya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo Julai 20, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 20 Julai, 2020 amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao imehudhuriwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu na viongozi wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Ad
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt Aloyce Nzuki kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo Julai 20, 2020

Rais Magufuli amewaapisha Mhandisi Marwa Mwita Rubirya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dkt. Aloyce Kashindye Nzuki kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhandisi Anthony Damian Sanga kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Dkt. Sief Abdallah Shekalaghe kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Allan Herbert Kijazi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhandisi Nadhifa Sadiki Kemikimba kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Dkt. Mwinyi Talib Haji kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhandisi Anthony Sanga kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo Julai 20, 2020

Aidha, Rais Magufuli ameshuhudia Wakuu wa Mikoa wakiwaapisha Wakuu wa Wilaya aliowateua katika Mikoa yao ambapo Mkuu wa Mkoa wa Geita Bw. Robert Gabriel Luhumbi amemuapisha Bw. Fadhili Mohamed Juma kuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Aboubakar Kunenge amemuapisha Bw. Mussa Ramadhan Chogero kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Anthony Mtaka amemuapisha Bw. Aswege Enock Kaminyoge kuwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Bw. Joachim Wangabo amemuapisha Bw. Calorius Constantine Misungwi na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Anna Mghwira amemuapisha Dkt. Athumani Juma Kihamia kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rombo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Seif Shekilage kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo Julai 20, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
akimuapisha Dkt Allan Kijazi kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Maliasili na Utalii kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani
Dodoma leo Julai 20, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akimuapisha Bw. Fadhili Mohamed Juma kuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita kwenye Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma Jumatatu Julai 20, 2020

Wateule wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya ambao ni Bw. Bashir Paul Mhoja (Iringa), Bw. Ramadhan Salmin Possi (Chalinze), Bw. Baraka Michael Zikatimu (Urambo), Bw. John John Nchimbi (Babati), Bw. Emmanuel Matinyi Johnson (Kishapu) na Bw. Solomon Isack Shati (Hanang).

Viongozi walioapishwa wakitia saini hati za Viapo vya Maadili ya Viongozi kwenye hafla iliyofanyikia Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma Julai 20, 2020

Pia, Makatibu Tawala wa Wilaya ambao ni Bi. Hanan Muhamed Bafagil (Arusha), Bw. Omary Mwanga (Nachingwea) na Bw. Saitoti Zelothe Stephen (Mbeya).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhandisi Nadhifa Kemikimba kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara yua Maji kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo Julai 20, 2020

Akizungumza baada ya kuwaapisha, Rais Magufuli amewataka viongozi hao kwenda kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na kwa kuzingatia viapo vyao na kwamba Watanzania wana matarajio makubwa nao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapongeza viongozi mbalimbali aliowaapisha kwenye Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma Jumatatu Julai 20, 2020

Mhe. Rais Magufuli amemuelezea kila kiongozi aliyeteuliwa na ametaka waende wakashirikiane na viongozi wengine katika maeneo waliyopangiwa ili kuwatumikia vizuri wananchi hasa kutatua kero zinazowakabili na kuimarisha upatikanaji wa huduma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akimuapisha Bw. Aswege Enock Kamichonge kuwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa kwenye Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma Jumatatu Julai 20, 2020

Ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa juhudi kubwa za kuimarisha mazingira ya utalii hapa nchini hali inayowavutia watalii wengi kuja kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo licha ya kuwepo ugonjwa wa Corona (Covid-19).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu Wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi John Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Dkt. Laurian Ndumbaro, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga na Dkt Laurian Ndumbaro wakiwa na viongozoi mbalimbali walioapishwa kwenye Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma Jumatatu Julai 20, 2020

Rais Magufuli amesema Tanzania ni salama na wanaotembelea Tanzania wanakuwa salama. Amevishukuru vyombo vya ulinzi na usalama kwa jitihada mbalimbali za kuimarisha usalama.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA ATEMBELEA RUKWA.. AANGAZIA AFYA, ELIMU, KILIMO NA MIUNDOMBINU KWA MIRADI YA MAENDELEO.

Katika ziara ya Rais Samia siku ya leo iliangazia kwenye sekta ya Afya, Elimu, Kilimo …

2 Maoni

  1. peregonavtofgtd kiev ua

    Быстро, сверхэффективно а также фундаментально провезти Чемодан автомобиль изо Украины на Европу, чи изо Европы на Украину вместе с нашей командой. Формирование грамот а также экспортирование производятся в течение оговоренные сроки.
    http://peregonavtofgtd.kiev.ua

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *