RAIS MAGUFULI ATAJA SABABU ZA KUOMBA TENA KUGOMBEA URAIS

Rais Dkt. John Magufuli amesema kuwa suala lililomfanya kuchukua fomu ya kugombea muhula wa pili ni kuendelea kuwatumikia watanzania kwa kuendelea na kazi aliyoianza.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Ofisi za CCM makao Makuu mjini Dodoma mara baada ya kutoka kuchukua fomu ya kugombea urais kwa awamu ya pili.

Ad
Mgombea urais kupitia CCM Rais Dkt. John Magufuli akiwa na Mgombea Mwenza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakiwa wameshika fomu za kuomba udhamini kwa watanzania ambapo wanatakiwa wadhamini 2000

“Wanaccm katika kufikiria haya kwamba tumehangaika hiki tukiondoka wale wenye rangi nyingine ambazo sio za kijana watakuja kweli kuyafanya haya waliokuwa wanashirikiana na mabeberu kutuibia madini yetu leo watangeuka wawe watu wema wa kutusaidia sisi watanzania ndio maana nimesema potelea mbali nagombea hii miaka mitano mengine watanzania wanipe hiyo” alisema Rais Magufuli

Aidha, Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania ni taifa tajiri lakini wananchi walizoeshwa kuambiwa Tanzania ni maskini na ndio sababu sasa Tanzania imingia uchumi wa kati.

Amesema sababu nyingine iliyomfanya kugombea ni kuhakikisha miradi yote aliyoianzisha inamaliziwa na kutoa matokeo chanya kwa Taifa ikiwemo kuanzisha viwanda vitakavyosaidia kuongeza ajira kwa watanzania na kuuza bidhaa nje badala ya kuuza malighafi.

kwa upande wake Mgombea Mwenza ambaye pia ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kwa kiasi kikubwa cha asilimia 74 tatizo ya maji limepungua Tanzania.

Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali imebeba jukumu la kuwalipia wananchi ada mzigo ambao ulikuwa unabebwa na kinamama lakini kwa sasa umepokelewa na serikali.

“Tunashukuru sana Mwenyekiti na zaidi ya yote umetungarisha katika manyumba yetu mpaka vijijini kwenye vitembe tunang’ara na umeme Mwenyekiti tunakushuru sana mengine ni ya jumla na kuna mengi yamefanywa yanatugusa wanawake” amesema Makamu wa Rais

Ad

Unaweza kuangalia pia

Msalaba Mwekundu: Nguzo ya Kibinadamu na Ujenzi wa Jamii Imara

Msalaba Mwekundu, ambao ni sehemu ya Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *