RAIS MAGUFULI APEWA TUZO MAALUM YA HESHIMA NA KANISA TA TAG

Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Tanzania (TAG) Dkt. Barnabas Mtokambali amesema kuwa Baraza kuu la Kanisa hilo limeamua kutoa Tuzo Maalum ya Heshima kwa Rais Dkt. John Magufuli.

Amesema hayo wakati wa kumkabidhi Rais Magufuli Tuzo hiyo katika mkutano wa Baraza kuu la Kanisa hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Biblia Miyuji jijini Dodoma leo tarehe 14 Agosti 2020

Ad
Rais Dkt John Magufuli akipokea Tuzo kwa ajili ya kumtengemea Mungu katika mapambano dhidi ya Corona kutoka kwa Askofu Mkuu Dkt. Barnabas Mtokamnali wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) mjini Dodoma

Dkt. Mtokambali amesema kuwa Baraza kuu la kanisa limeamua kutoa tuzo hiyo kutokana jinsi Rais Dkt. Magufuli alivyoongoza Taifa kumtengemea Mungu katika kipindi kigumu cha janga la ugonjwa wa virusi vya corona.

“Wakati mataifa mengine yakiweka nguvu kwenye kuwazuia watu wao wasitoke manyumbani (lockldown) na kufunga shughuli mbalimbali za kuletea mataifa yao maendeleo wewe umefanya mambo tofauti kabisa duniani” amesema Dkt. Mtokambali

Dkt. Mtokambali amesema kuwa kitendo cha Rais Magufuli kutowafungia watu ndani na kuwaelekeza wafanye kazi na kumtafuta Mungu wao kwa bidii ambaye ndiye jawabu la kweli la mambo yote kumeliweka Taifa kwenye nafasi ya kipekee sana duniani katika kumtengemea Mungu na kulifanya Taifa kutoyumba kiuchumi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Msalaba Mwekundu: Nguzo ya Kibinadamu na Ujenzi wa Jamii Imara

Msalaba Mwekundu, ambao ni sehemu ya Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *