NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU PROF. JAMES MDOE ATETA NA MENEJIMENTI YA BODI YA MIKOPO

Ismail Ngayonga, Dar es salaam

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe leo (Jumatatu, Agosti 31, 2020) amefanya ziara ya kikazi katika ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Jijini Dar es Salaam ili kukagua utendaji kazi na kuwataka watumishi wa HESLB kuendelea kuchapa kazi.

Ad

Katika ziara hiyo, Prof. Mdoe alikutana na menejimenti ya HESLB ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Abdul-Razaq Badru ambao walimueleza kiongozi huyo kuwa wanaendelea kupokea maombi mikopo ya elimu ya juu kutoka kwa wanafunzi hadi Septemba 10 mwaka huu.

2. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe (kulia) akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe wakati wa ziara yake ya kikazi katika Ofisi za HESLB ambapo alizungumza na menejimenti ya HESLB iliyoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji leo Jumatatu (Agosti 31, 2020). Kushoto ni Mkuu wa MawasilianO HESLB, Omega Ngole. (PICHA NA BODI YA MIKOPO- HESLB)

“Nimekuja kuona mmejiandaaje na mwaka mpya wa masomo na hali ya uombaji mikopo inavyoendelea na nimefurahi kusikia mnaendelea vizuri, endeleeni kuchapa kazi,” amesema Prof. Mdoe katika kikao kazi na wajumbe wa menejimenti ya HESLB kilichofanyika katika ofisi za HESLB zilizopo eneo la TAZARA.

Akizungumza katika kikao hicho, Badru alisema watumishi wa HESLB wanaendelea vizuri na majukumu yao na kuwa kufuatilia kupokea maoni ya wadau, HESLB imeamua kuongeza muda wa kupokea maombi ya mikopo kutoka kwa wanafunzi hadi Septemba 10 mwaka huu.

“Mwisho ilikua iwe leo saa sita usiku, lakini tumeamua kuongeza siku kumi ili kuwawezesha wateja wetu ambao hawajakamilisha maombi yao kufanya hivyo,” amesema Badru na kuongeza kuwa uamuzi huo umefuatia mashauriano na wadau wengine kama Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) na Shirika la Posta Tanzania (TPC) ambazo nazo zinawahudumia wateja hao.

Kuhusu malipo kwa wanafunzi waliopo vyuoni, Badru amesema TZS 15.57 bilioni zimetumwa vyuoni kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi wanufaika 39,721 kuendelea na mafunzo kwa vitendo katika maeneo mbalimbali kuanzia wiki hii.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Je! Wajua Mchango wa Madini ya Tanzanite katika Pato la Taifa?

Madini ya Tanzanite, yanayopatikana pekee katika eneo dogo la Mererani, Tanzania, ni miongoni mwa rasilimali …

7 Maoni

  1. Профессиональные seo https://seo-optimizaciya-kazan.ru услуги для максимизации онлайн-видимости вашего бизнеса. Наши эксперты проведут глубокий анализ сайта, оптимизируют контент и структуру, улучшат технические аспекты и разработают индивидуальные стратегии продвижения.

  2. You have a source of the latest and most interesting sports news from Kazakhstan: “Kazakhstan sports news https://sports-kazahstan.kz: Games and records” ! Follow us to receive updates and interesting news every minute!

  3. Find out how Pedri https://barcelona.pedri-cz.com becomes a key figure for Barcelona – his development, influence and ambitions determine the club’s future success in world football.

  4. Follow Liam Neeson’s career https://hostage.liam-neeson.cz as he fulfills his potential as Brian Mills in the film “Taken” and becomes one of the leading stars of Hollywood action films.

  5. Пансионаты для пожилых людей https://moyomesto.ru в Самаре по доступным ценам. Специальные условия по уходу, индивидуальные программы.

  6. Bieber’s https://baby.justinbieber-br.com path to global fame began with his breakthrough success Baby, which became his signature song and one of the most popular music videos of all time.

  7. Roberto Firmino https://al-ahli.roberto-firmino-ar.com one of the most talented and famous Brazilian footballers of our time, has paved his way to success in different leagues and teams.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *