SERIKALI INATENGENEZA MAZINGIRA MAZURI KWA WAWEKEZAJI – WAITARA

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mwita Waitara amesema Serikali inatengeneza mazingira mazuri kwa wawekezaji wanaofuata sheria.

Waitara ametoa kauli hiyo leo Desemba 23, 2020 alipotembelea kiwanda cha Saji Packaging kinachojihusisha na uzalishaji wa vifungashio vya plastiki na kurejeleza taka za plastiki kilichopo Iliemela jijini Mwanza.

Ad

Akionesha kuridhishwa na shughuli za kiwanda hicho alisema ni rafiki kwa mazingira kutokana na kukusanya taka za plastiki ambazo zingezagaa ovyo na kuzitumia kama malighafi.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mwita Waitara (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa kiwanda cha Salim Khahi kilichopo wilayani Ilemela jijini Mwanza kinachojishughulisha na uzalishaji wa vifungashio na kurejeleza taka za plastiki.

“Kazi ya Serikali ni kuhakikisha pia mnazingatia kanuni, sheria, taratibu na miongozo mbalimbali na mkifanya hivyo wala hatutagombana na tumekuja hapa tumeona mnafanya kazi vizuri bila kuathiri maziangira,” alisema.

Aidha amewataka wamiliki wengine wa viwanda kufuata utaratibu na pindi wanapokwama katika shughuli zao wasisite kuomba ushauri kutoka mamlaka husika zikiwemo Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Kwa upande wake Mkaguzi kutoka TBS Kaanda ya Ziwa, Nelson Mugema alitoa wito kwa wenye viwanda wengine kuthibitisha ubora wa bidhaa katika shirika hilo.

Mugema alisema kuwa TBS imendaa viwango mbalimbali katika vifungashio vya vyakula na bidhaa nyingine zikiwemo mikate ambavyo vinamfikia mlaji wa mwisho.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mwita Waitara akiangalia mojawapo ya mashine za uzalishaji wa vifungashio vya plastiki alipotembelea kiwanda cha kilichopo wilayani Ilemela jijini Mwanza. (PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

Kama ambavyo Serikali ilivyopiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia Juni mosi 2019, aliwataka wafuate utaratibu kwa kupeleka maombi ili vifungashio wanavyozalisha vithibishwe ubora tayari kwa kupelekwa sokoni na kulinda mazingira.

Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Salim Khahi aliishukuru Serikali kupitia watendaji wake ambao amekuwa akiwapa ushirikino katika suala zima la hifadhi ya mazingira.

“Hapa katika kiwanda hiki mazingira yanalindwa vizuri na kiwanda hiki hakizalishi uchafu wa aina yoyote na hatutupi taka ya aina yoyote zote tunazikusanya hapa na tunazifanyia recycling (kurejeleza),” alisema Khahi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

USHAWISHI WA TANZANIA DUNIANI UTATEGEMEA NA UBORA WA SERA YA MAMBO YA NJE INAYOREKEBISHWA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu-Zanzibar, Mhe.  Ali Suleiman Ameir akitoa hotuba ya ufunguzi ya …

Oni moja

  1. Cograturation for gretest work

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.