MHANDISI KUNDO AZINDUA VISIMA 20 VYA MAJI BARIADI

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi akichota Maji kwenye kijiji cha Bubale kilichopo Kata ya Nkololo, Bariadi kabla ya uzinduzi wa visima sita vya maji jimboni humo

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Andrea Mathew ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi, amezindua visima 6 vya maji kwenye Kata tatu za jimbo hilo ikiwemo kata ya Ihusi, Nkololo na Mwaumatondo ambapo kila kata imepata visima viwili

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye ni Mbunge wa Bariadi akisukuma maji akiwa kijiji cha Bubale kilichopo Kata ya Nkololo, Bariadi kabla ya uzinduzi wa visima sita vya maji

Ujenzi wa visima hivyo ni mwendelezo wa kampeni ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya Kumtua Mama Ndoo Kichwani ili kuongeza upatikanaji wa maji karibu na makazi ya wananchi na kupunguza adha kwa wanawake ya kutumia muda mwingi kutafuta maji ili kuwapa wananchi fursa ya kufanya majukumu mengine katika jamii zao ili kujiongezea kipato

Ad

Uzinduzi huo umefanyika kwenye kijiji cha Bubale kilichopo Kata ya Nkololo ambapo amemtweka ndoo ya maji kichwani Nkwimba Maduhu, mmoja wa wakazi wa kijiji hicho wa niaba ya wanawake wengine na wananchi waishio kijijini hapo

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi akinywa maji ya kisima kwenye kijiji cha Bubale kilichopo Kata ya Nkololo, Bariadi kabla hajazindua visima sita vya maji jimboni humo

Mhandisi Kundo ameongeza kuwa uchimbaji na ujenzi wa visima vingine 20 unaendelea kwenye Kata ya Dutwa na Ngulyati na atavindua mara baada ya kukamilika

Ad

Unaweza kuangalia pia

Makamu wa Rais Dkt. Mpango Awakaribisha Wawekezaji Katika Nishati ya Jotoardhi Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewakaribisha wawekezaji …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *