NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI ATOA SIKU 60 KWA SUMA JKT KUKAMILISHA UJENZI WA TENKI LA MAJI BUIGIRI

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji mhandisi Nadhifa Kemikimba ametoa siku 60 kwa mkandarasi SUMA JKT anayejenga tenki la maji katika eneo Buigiri wilayani Chamwino kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo ili wananchi wapate huduma ya maji.

Tanki hilo lenye ujazo wa wa lita Milioni 2.5 linajengwa kwa gharama ya Sh Milioni 998 na linatarajiwa kuhudumia wakazi wa Chamwino Ikulu,Hospitali ya Uhuru na Buigiri.

Ad

Akizungumza akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali ya maji,mhandisi Nadhifa amesema tenki hilo lilitakiwa lijengwe mwezi septemba mwaka jana lakini limechelewa kukamilika.

“Tumekubaliana na mkandarasi kuwa tenki hili likamilike ndani ya miezi miwili,ili kuharakisha kazi hii menejimenti ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) fuatilieni kazi hii kila siku ili mradi ukamilike kwa wakati,”aliagiza Naibu Waziri huyo.

Mbali na mradi huo,Mhandisi Nadhifa ametembelea eneo la Ihumwa panapochimbwa visima,ametembelea eneo la Nzughuni kunapofufuliwa kisima ambapo amesema ameridhishwa na utendaji kazi wa DUWASA .

“Hapa nimeridhishwa na menejimenti ya DUWASA,wamefanya jitihada kubwa ya kuhakikisha wananchi wanapata maji,kazi inayofanyika hapa ni kufufua visima ambavyo vilichimbwa zamani ni ubunifu mkubwa,hongereni sana,”alipongeza.

Akizungumza katika eneo hilo,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo mhandisi Aron Joseph amesema dhamira waliyonayo ni kuvifufua visima vya zamani ili visaidie kutoa huduma na mpaka sasa wameshavitambua visima 11 vilivyopo katikati ya mji.

“Kisima hiki kilikuwepo tangu mwaka 1989 lakini kutokana na changamoto mbalimbali kilitelekezwa,dhamira yetu ni kuvitambua na kuvifufua visima hivi ili viweze kusaidia kutoa huduma ya maji kwa wananchi na hivyo kupunguza upungufu wa maji uliopo,”alisema Mhandisi huyo.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Mitazamo ya Uongozi ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu katika Sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii, na Haki za Watoto

Ummy Ally Mwalimu ameonyesha mitazamo ya uongozi yenye mwelekeo wa kujali maendeleo na ustawi katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *