WAZIRI MWAMBE AWATAKA WATUMISHI WA BARAZA LA USHINDANI (FCT) KUFANYA KAZI KWA WELEDI

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe (Mb) aliwasihi  wafanyabiashara kuwasilisha rufaa zao iwapo hawakuridhika na maamuzi yanayotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (EWURA, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri na Usalamawa Anga (TCAA), Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu LATRA, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa juu wa Petroli (PURA) pamoja na mamlaka ambazo sheria za uundaji wake zinaelekeza rufaa za maamuzi yake zifanywe na FCT.

Waziri Mwambe aliyasema hayo alipokuwa akiongea na menejimenti na wafanyakazi wa FCT alipofanya ziara katika Baraza hilo akiambatana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa Wizara ya Viwanda na Biashara.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe (Mb) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Baraza la Ushindani, akiambatana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) wa kwanza kulia naye akisaini kitabu cha wageni. Aliyesimama katikati ni Msajiri wa Baraza la Ushindani Bw. Renatus Rutatinisiwa.

Akiwa katika ziara hiyo katika baraza hilo lenye jukumu la kupokea,kusikiliza na kuamua kesi za rufaa zinazotokana na maamuzi ya Tume ya Ushindani (FCC) pamoja na Mamlaka za Udhibiti, Mhe Waziri alisema  wananchi wasiogope kwenda kutafuta haki katika baraza hilo ambalo limepewa hadhi ya kimahakama ya utoaji haki kwenye masuala ya ushindani udhibiti wa soko, kumlinda mlaji  na maamuzi ya kesi za rufaa yanayotolewa na baraza hilo ni ya mwisho.

Aidha Waziri Mwambe aliwataka amewataka watumishi wa Baraza la Ushindani (FCT) kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kuepuka vitendo vya rushwa wakati wakiwahudumia wafanyabiashara wanaofika katika baraza hilo kutafuta haki katika kesi zinazohusu biashara zao na wajiendeleze kielimu ili kuendana na wakati.

Naye Naibu Waziri akiongea na watumishi wa baraza hilo  aliwapongeza kwa kufanya kazi vizuri na aliwaahidi kuwa Wizara ya Viwanda itaendelea kushirikiana na Baraza hilo ambalo ni muhimu katika kuendeleza biashara nchini ili kuliwezesha kufanya kazi  kwa ufanisi.

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUMSHUSHA MAMA NDOO KICHWANI – MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilwa, kufanya utafiti wa kina …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.