MAJALIWA – SERIKALI IMEDHAMIRIA KUFUFUA ZAO LA MKONGE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kufufua zao la mkonge nchini, hivyo amewataka Watanzania wachangamkie fursa hiyo  kwa kujenga viwanda vya kuchakata bidhaa mbalimbali zitokanazo na zao hilo kama sukari, dawa, vinywaji, mbolea na nyuzi.

Ametoa kauli hiyo Alhamisi, Januari 21, 2021 wakati akizungumza na wananchi baada ya kukagua shamba la mkonge la Kigombe wilayani Muheza ambalo ni miongoni mwa mashamba ya mkonge yaliyo chini ya Kampuni ya Amboni Plantation Limited.

Ad

Waziri Mkuu amesema wakati umefika kwa Watanzania wanaoishi katika maeneo ambayo zao la mkonge linastawi wachangamkie fursa hiyo kwa sababu zao hilo linalimwa na watu wote na si kilimo cha matajiri peke yake.

Amesema awali watu waliaminishwa kwamba zao la mkonge ni zao linalolimwa na watu wenye uwezo mkubwa mkubwa kifedha na wengine walibaki kuwa vibarua jambo ambalo si kweli. “Wote tunaweza kulima mkonge na Serikali imejipanga kuhakikisha zao hili linalimwa na watu wote, amua sasa na utaona faida yake.”

“Mkonge ni utajiri, mkonge ni fedha ya uhakika na mkonge ni zao ambalo mzazi akiwekeza kwa ajili ya mtoto wake litamsaidia hapo baadaye hata kama yuko darasa la saba, mkonge atakaoupanda leo utamsomesha hadi chuo kikuu.”

Waziri Mkuu amesema kwamba mkulima wa kawaida anaweza kuanza kulima hata ekari moja, ambayo atapanda jumla ya miche 1,600 na baada ya miaka mitatu atavuna tani moja na nusu hadi mbili iwapo shamba litasimamiwa vizuri. Bei ya tani moja ya mkonge wa daraja la juu ni sh. milioni nne.

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwataka vijana kujikita katika kilimo hicho na pia waanzishe vitalu vya miche ya mkonge na kuiuza kwa wakulima kwa sababu mahitaji yameongezeka baada ya Serikali kufufua zao hilo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Amboni Plantation Limited, Casbert Nail amesema wameajiri watumishi 2,490 katika mashamba yao matatu, Mwera Estate (901), Sakura Estate (832) na Kigombe Estate (757).

Ad

Unaweza kuangalia pia

Makamu wa Rais Dkt. Mpango Awakaribisha Wawekezaji Katika Nishati ya Jotoardhi Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewakaribisha wawekezaji …

4 Maoni

  1. Discover the fascinating world of online games with GameHub Azerbaijan https://online-game.com.az. Get the latest news, reviews and tips for your favorite games. Join our gaming community today!

  2. Conor Anthony McGregor https://conor-mcgregor.com.az Irish mixed martial arts fighter who also performed in professional boxing. He performs under the auspices of the UFC in the lightweight weight category. Former UFC lightweight and featherweight champion.

  3. Harry Kane’s journey https://bavaria.harry-kane-cz.com from Tottenham’s leading striker to Bayern’s leader and Champions League champion – this is the story of a triumphant ascent to the football Olympus.

  4. Try to make a fascinating actor Johnny Depp https://secret-window.johnny-depp.cz, who will become the slave of his strong hero Moudriho Creeps in the thriller “Secret Window”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *