WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, DKT.NDUMBARO AWATAKA WAKAZI WA MKOA WA LINDI KUCHANGAMKIA FURSA ZA UTALII

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amewataka Wakazi wa Mkoa wa Lindi kuchangamkia fursa za utalii zilizopo katika mkoa huo.

Ameyasema hayo wakati alipotembelela Hifadhi ya urithi wa utamaduni  wa Dunia Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songomnara ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli.

Ad

Amesema kazi ya serikali sio kutoa pesa kwa mtu mmoja mmoja bali kazi yake ni kutengeneza fursa ili wananchi waweze kuendesha shughuli za kiuchumi kutokana na fursa zinazopatikana katika eneo hisika.

Amesema mkoa wa Lindi hasa wilaya ya Kilwa umejaliwa kuwa na aina lukuki za  utalii  ikiwemo vivutio vya utalii vya mambokale, uwindaji wa kitalii, utalii wa fukwe pamoja na  utalii wa picha.

Ameongeza kuwa Mkoa wa Lindi unashika nafasi ya pili katika mikoa yenye maeneo ya misitu mikubwa nchini ikiongozwa na mkoa wa Katavi ambao una asilimia 82.7 ya eneo lake limefunikwa na misitu.

” Nimeamua kuanzia ziara yangu  katika mkoa huu ili kuja  kuwambia   Wana Kilwa mmekaa juu ya dhahabu changamkeni ‘” amesisitiza Ndumbaro.

Akizungumza na Wakazi hao wa Kilwa Kisiwani, Dkt. Ndumbaro amewataka Wananchi hao kichangamkia fursa  hizo  zinazoambatana na utalii kama vile chakula,  usafiri, huduma za malazi pamoja na ngoma za asili baadala ya kuwa Walalamikaji.

” Shida tuliyo nayo sisi tunapenda vitu virahisi rahisi na tumekuwa sio watu wa kupambana na tumekuwa tukichukua muda mwingi kuilaumu Serikali badala ya kuzitumia fursa hizi. Alisisitiza Dkt.Ndumbaro.

Amewataka Wananchi hao kubadilika na kuanza kuchangamkia  fursa nyingi zilizopo ili waweze kuwa matajiri.

” Sisi Wizara ya Maliasili na Utalii tumewaletea Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) ili kuboresha maeneo ya vivutio vya utalii vya Mambokale  ili wananchi mpate na serikali ipate pia ” amesisitiza Dkt.Ndumbaro.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA,  Maj.Gen ( Mst) Hamisi  Semfuko amewataka wakazi hao kuwa mstari wa mbele katika kulinda na kuviendeleza vivutio vya kihistoria vya utalii ili viweze kuwasaidia kiuchumi.

Amesema moja ya hatua ambazo TAWA wamezichukia katika magofu hayo  ni kununua boti mpya ya kisasa kwa ajili ya usafiri kwa watalii pamoja na kuweka miundombinu wezeshi kwa ajili ya watalii kutembelea eneo hilo.

Awali Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilwa Kisiwani, Shabani Ali ameishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia TAWA kwa kuyakarabati magofu hayo ambayo yalikuwa kwenye hali mbaya

” Kwa sasa tumeanza kuona matunda ya magofu haya Watalii  wamekuwa wakitembelea kwa wingi katika maeneo haya tofauti na kipindi cha nyuma kabla ya ujio wa TAWA.

Ad

Unaweza kuangalia pia

TRENI YA MCHONGOKO YAANZA SAFARI KWA KISHINDO DAR – DOM

Treni ya Umeme ya Kisasa (EMU) ya Reli ya Kisasa (SGR) nchini Tanzania ni sehemu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *