NIMEDHAMIRIA KUENDELEZA JITIHADA ZA KUTATUA CHANGAMOTO ZA MUUNGANO ZILIZOBAKIA – WAZIRI UMMY MWALIMU

Na Lulu Mussa, Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Ummy Mwalimu hii amefanya ziara ya kikazi visiwani Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha.

Ad
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Ikulu Zanzibar mara baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha. Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Khalid Salum Mohammed (kulia) na Balozi Mbarouk Mbarouk Mkurugenzi Idara ya Muungano.

Waziri Ummy amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi Ikulu Zanzibar. Katika mazungumzo yao Mwalimu amesema kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Zanzibar amedhamiria kuendeleza jitihada za kutatua changamoto za Muungano zilizobakia.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Ikulu Zanzibar. Waziri Ummy Mwalimu yuko visiwani Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha.

“Rais nikuhakikishie kuwa nitafanya kazi kwa karibu sana na Mhe. Khalid Waziri mwenzangu kuhakikisha hoja ambazo bado hazijapatiwa ufumbuzi zinafanyiwa kazi na mwanzoni mwa mwezi Januari tunategemea kuwa na kikao cha pamoja baina yetu” Alisisitiza Mhe. Ummy.

Kwa upande wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amempongeza Ummy Mwalimu wa kuteuliwa tena kuwa Waziri na kusisitiza kuwa Serikali yake itampa ushirikiano katika kuratibu masuala ya Muungano.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Maalim Seif Shariff Hamad mara baada ya mazungumzo hii leo Visiwani Zanzibar, Waziri Mwalimu yuko Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha

Katika hatua nyingine Waziri Ummy Mwalimu amefanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharrif Hamad Chukwani Zanzibar.

Mhe. Hamad amesisitiza umuhimu wa Wizara zenye hoja za Muungano kukutana na kutafuta suluhu ya mapema na kuhamasisha  Wizara zisizo na hoja kukutana pia kwa lengo la kudumisha undugu baina ya  Tanzania bara na Tanzania Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Maalim Seif Shariff Hamad mara baada ya mazungumzo baina yao hii leo Visiwani Zanzibar.

“Nashauri na kusisitiza Wizara zinazoshabihiana zikutane na kuhakikisha hoja zinazopatiwa ufumbuzi zitekelezwe ipasavyo” alisisitiza Maalimu Seif Sharif Hamad.

Waziri Ummy Mwalimu yuko visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na hapo kesho atatembelea miradi ya Muungano inayotekelezwa pande zote mbili.

Ad

Unaweza kuangalia pia

TRENI YA MCHONGOKO YAANZA SAFARI KWA KISHINDO DAR – DOM

Treni ya Umeme ya Kisasa (EMU) ya Reli ya Kisasa (SGR) nchini Tanzania ni sehemu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *