Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo (Jumanne, Januari 5, 2020) amezindua rasmi safari ya meli mpya ya MV Mbeya II katika Bandari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa itakayotoa huduma katika Ziwa Nyasa nchini na nchi jirani za Msumbuji na Malawi.
Meli hiyo yenye thamani ya shilingi bilioni 9.1 ni muendelezo wa Serikali ya Awamu ya Tano wa kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji wa mizigo na abiria kwa lengo la kuboresha uchumi.
Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri Mkuu amewataka wananchi waitunze meli hiyo
Ad
Aidha, Waziri Mkuu amesema Tanzania imezungukwa na nchi nane ambazo zinategemea kupata bidhaa mbalimbali kutoka nchini hivyo Wananchi watumie fursa ya uwepo wa meli hii kufanya biashara.
Amesema wananchi hawawezi kupata maendeleo bila ya Serikali kujenga miundombinu kama ya meli, barabara, bandari, hivyo amewataka waitumie vizuri kwa ajili ya kukuza uchumi wao.
Meli hiyo imejengwa na kampuni ya Kitanzania ya Songoro Marine