MBUNGE RIDHIWANI KIKWETE AMPONGEZA NA KUMSHUKURU FLAVIANA MATATA KWA KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU CHALINZE

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amempongeza na kumshukuru Mwanamitindo wa Kimataifa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Matata, Bi.Flaviana Matata kwa kujitoa kwake kusaidia masuala ya elimu ndani ya Jimbo hilo.

Awali akizungumza wakati wa kutoa shukrani zake kwa mwanamitindo huyo, Mbunge Ridhiwani Kikwete alisema wameupokea kwa mikono miwili huku akimuomba kuendelea kusaidia bila kuchoka na maeneo mengine.

Ad
Wanafunzi wa shule ya msingi Msinune wakifurahia baada ya kupokea zawadi ya mabegi ya shule

“Tunakupongeza sana kwa misaada hii unayotoa kwetu haswa kijiji hiki cha Msinune. Sisi tutaendelea kukuombea dua njema na kukupa ushirikiano mkubwa kuhakikisha kuwa malengo ya taasisi yako yanafikiwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Wananchi wetu wanafaidika na uwepo wa Taasisi yako”.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa na Flaviana Matata pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Msinune wakionyesha taulo za kike zilizotolewa na Flaviana Matata Foundation

Mbunge Kikwete, alimuhakikishia Bi. Flaviana Matata kuwa Ofisi yake na Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, inatambua michango yako katika shule hii ikiwemo kusaidia ujenzi wa nyumba za walimu, madarasa, vyoo na hata maji na leo hii vifaa vya shule kwa wanafunzi wetu

Aidha, Mbunge alimhakikishia Bi.Flaviana kuwa atamuunga mkono katika ujenzi wa nyumba za walimu.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa na Flaviana Matata pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Msinune baada ya kupatiwa mabegi ya shule kutoka kwa Taasisi ya Flaviana Foundation

“Mimi kama Mbunge lazima nikupatie sapoti kwa hatua hii. Pili sisi kama Halmashauri na kupitia mfuko wa Jimbo nipo tayari kusaidia vifaa vya ujenzi ilikukamilisha nyumba za walimu ili kuboresha elimu yetu”. alisema Ridhiwani Kikwete.

Kwa upande wake, Flaviana Matata amewashukuru Walimu, Kamati ya shule, Diwani wa Kata hiyo pamoja na Mbunge kwa namna wanavyotoa ushirikiano mkubwa hali ambayo amewaahidi kuendelea kusaidia juhudi hizo bila kuchoka.

Wanafunzi wa shule ya msingi Msinune wakifurahia baada ya kupokea zawadi ya mabegi ya shule

Andrew Chale, Chalinze

Aidha, Flaviana Matata alimhakikishia Mbunge Ridhiwani Kikwete kuendelea kuchangia elimu ikiweo kuendeleza ujenzi wa nyumba za walimu na miundombinu mingine akiwa kama mlezi wa shule hiyo.

Katika hatua nyuingine, Flaviana Matata aliwaomba wazazi kuacha tabia ya kuwataka watoto wa kike kuwasimamisha masomo na baadala yake amewataka waache wasome ilikuja kuwa msaada kwao hapo.

Katika tukio hilo, zaidi ya Wanafunzi 300 waliweza kukabidhiwa begi za shule sambamba na taulo za kike zilizogaiwa kwa baadhi ya wanafunzi wa darasa la Saba, kutoka kwa Taasisi hiyo.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Serikali ya Tanzania na Czech Zakubaliana Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili

Serikali za Tanzania na Czech kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kuvutia uwekezaji kati yao. Kuondoa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *