- Zaidi ya kiasi cha shilingi milioni 125 zimekusanywa na Wafugaji katika tarafa ya Ngorongoro wakishirikiana na Viongozi wa kisiasa na Taasisi za umma na binafsi ambazo zitatumika kuimarisha vikundi vya kuweka akiba na kukopa (Vikoba ) ili kusaidia kaya masikini kujikwamua kiuchumi.
- Edward Maura ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji kutoka vijiji vya tarafa ya ngorongoro amesema kuwa wamekutana na kuanza kuchanga zaidi ya shilingi milioni miamoja huku wengine wakijitolea mbuzi ng’ombe na kondoo, wafikika hatua hiyo baada ya kuona kuwa hakuna sababu ya kusubiri misaada kutoka nje wakati wenyewe wanauwezo wa kutatua changamoto zao kwa kuunganisha nguvu pamoja.
- William Ole Nasha ni Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Ngorongoro amesema kuwa hatua ya kusaidia vikundi hivyo itasaidia katika kupunguza umasikini kwa wafugaji hao kwa kutumia Vikoba ambavyo vimekua vikileta matokeo makubwa katika uchumi wa wananchi.
- James Ole Millya ni Mbunge wa Simajiro amesema kuwa uwezweshaji wa kundi la wafugaji wanaoshi katika mamlaka hiyo utasaidia pia katika kuibua vyanzo vipya vya mapato mbali na mifugo na pia na pia kuona umuhimu wa kuhifadhi rasilimali za wanyamapori na mazingira.
- “Wafugaji wamekua wahifadhi wakubwa katika maeneo ya hifadhi hivyo wanapaswa kuthamaniwa na kuwezeshwa kiuchumi ili waone matunda ya uhifadhi” Alisema Millya
- Amina Mollel ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha amesema kuwa juhudi za kuwawezesha wanawake kwa njia ya mikopo yenye riba nafuu zinapaswa kupewa kipaumbele na serikali imekua ikitoa fedha hizo za asilimia 10% kwa wanawake na vijana .
- Profesa Abiudi Kaswamila ni Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro eneo wanaloishi wafugaji hao anasema mpango huo utaleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa jamii hiyo. Na Vero Ignatus,Arusha.
Ad