ZANZIBAR…!

Wananchi wa Zanzibar wanahimizwa kuendelea kujitokeza kwenda kufanya uhakiki wa taarifa zao muhimu zinazohusu Utambulisho, Vizazi, Vifo, Talaka na Ndoa.

Zoezi hilo litakalofanyika kwa miezi mitatu, linafanyika kidigitali, kazi ambayo inafanywa na Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar ambapo taarifa zote zitahifadhiwa kidogitali kwa teknolojia ya kisasa kwa lengo la kumsaidia mwananchi yaani Mzazibari kutambulika katika sehemu zote muhimu zinazotoa huduma za kijamii kama hospitali, benki, usafiri, katika Mashirika ya Bima na katika kumbukumbu za uzazi na vifo.

Ad

Uhakiki na usajili huu umezinduliwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein Agosti 04, 2018 na shughuli za uandikisha zikaanza rasmi Septemba 08, 2018 katika vituo 11 ambavyo vimejengwa kila wilaya.

#SisiNiTanzaniaMpyA+

Ad

Unaweza kuangalia pia

ZANZIBAR NA ANGOLA KUSHIRIKIANA KWENYE SEKTA YA UTALII

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameupongeza uwamuzi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *