LATE LIVE: WAZIRI MKUU AKIZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KISHA WANANCHI WA UKARA

  • Aelezea agizo la Mhe. Rais kuhusu kutangazwa kwa tenda ya haraka sana kujengwa kwa kivuko kikubwa kitakachokuwa kikitoa huduma eneo la Ukara
  • Azungumza na wanachi na kuwasihi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba. Awaahidi kuwa rambirambi zote zinazokusanywa na serikali, zitakuwa za wafiwa na kiasi kidogo kuwa sehemu ya ujenzi wa mnara wa kumbukumbu ya ajali hii kubwa katika eneo walipozikwa abiria waliopoteza maisha katika ajali hiyo.
  • Awasihi wananchi kuepuka wapotoshaji wanaowayumbisha kwa taarifa sisizo sahihi. Asema serikali imejipanga vyema kushughulikia tatizo hilo kitaalamu na taarifa sahihi wakati wote zitatolewa na serikali kila inapolazimu.
  • Afafanua hatua mbalimbali za kiuchunguzi zinachukuliwa na serikali ili kubaini sababu mahsusi ya ajali pamoja na dosari zilizopo kwenye utaratibu mzima wa uendeshaji wa usafiri wa majini nchini.
  • Ashuhudia zoezi la kukinasua kivuko cha MV Nyerere kilichozama kazi inayofanywa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) chini ya usimamizi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo.
  • Mhe. Waziri Mkuu asisitiza kuwa atakuwepo eneo la tukio kwa siku zote mpaka zoezi zima la uokoaji, mazishi na kukinasua kivuko kilichozama litakapokamilika.

Fuatilia Waziri Mkuu Mhe. Kasim Majaliwa alipokuwa akizungumza muda mfupi uliopita kwa kubofya link ifuatayo;

Katika hatua nyingine, Mhe. Waziri Mkuu ameunda tume ya watu saba (7) kuchunguza ajali hiyo. Tume hiyo inaongozwa na Jenerali Mstaafu George Waitara. Wajumbe wa tume hiyo ni pamoja na Mbunge wa Ukerewe (CDM)  Mhe. Joseph Mkundi, Aliyekuwa Mtendaji mkuu TEMESA Mhandisi Celina Magessa, Wakili Julius Kalolo ambaye atasaidia mapitio ya sheria.

Ad

Wengine ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Queen Mlozi ambaye atasimamia stahili za akina mama, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Camillius Wambura na Bashiru Hussein kutoka ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Maafa.

Waziri Mkuu ameiagiza Tume hii kuanza kazi mara moja baada ya kuiunda.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MKUCHIKA: KILA MMOJA ANA JUKUMU LA KUPAMBANA NA RUSHWA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utwala Bora, Kapteni, George Mkuchika amewataka wananchi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *