MATAIFA ZAIDI YA 75 YASHIRIKI KONGAMANO LA MAFUTA NA GESI

  • Serikali imesema imejipanga vema kuhakikisha sekta ya nishati na hasa ya mafuta na gesi inawanufaisha Watanzania wote na kwamba nchi imefanya maandalizi makubwa kwa ajili ya kunufaika na sekta hiyo.
  • Hayo yamesemwa  jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Muungano January Makamba wakati akifungua kongamano la pili la wadau wa sekta ya mafuta na gesi wakati anamwakilisha mgeni rasmi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
  • Kongamano hilo limehudhuriwa na zaidi ya wadau 200 kutoka mataifa zaidi ya 75 duniani na moja ya ajenda ni kuangalia fursa ambazo zinaweza kupatikana katika sekta ya mafuta na gesi huku pia kongamano hilo likijita kuangalia fursa ambazo watanzania watanufaika nazo kutokana na uwepo wa miradi mikubwa inayoendelea nchini.
  • Waziri Makamba amesema ujumbe wa Waziri Mkuu katika kongamano hilo ni kwamba nchi imefanya maandalizi makubwa kwa ajili ya kunufaika na sekta ya gesi na mafuta.
OIL & GAS CONGRESS 01.png

Baadhi ya washiriki wa kongamano wa mafuta na gesi wakisikiliza maada kuhusu sekta hiyo.

OIL AND GAS CONGRESS JANUARY.png
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Muungano January Makamba akizungumza wakati akifungua kongamano la pili la wadau wa sekta ya mafuta na gesi jijini Dar es Salaam kuhusu kongomano la wadau wa mafuta na gesi.
OIL & GAS CONGRESS SALAMA ABOUD ZNZ.png

Waziri wa wizara ya Ardhi, nyumba, maji, nishati na mazingira Zanzibar, Salama Aboud Talib akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu kongomano la wadau wa mafuta na gesi.

Ad

OIL & GAS CONGRESS 02.png

OIL & GAS CONGRESS SUBIRA MGALU.png

Naibu waziri wa wizara ya nishati, Subira Mgalu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu kongomano la wadau wa mafuta na gesi.

OIL & GAS CONGRESS ABDULSAMAD ABDULRAHIM.png
Muandaaji wa kongamano la mafuta na gesi ambaye pia ni Mwanzilishi na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Watoa Huduma za Mafuta na Gesi nchini Tanzania Abdulsamad Abdulrahim akifafanua jambo.
Ad

Unaweza kuangalia pia

TANZANIA NA ANGOLA ZAJADILI USHIRIKIANO KATIKA MAFUTA NA GESI

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amekutana na Balozi wa Angola nchini Tanzania, Sandro De …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *