WAZIRI MKUU AIPONGEZA TFDA KWA KUIFANYA TANZANIA KUWA YA KWANZA KATIKA UDHIBITI WA UBORA

  • Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) inafanya kazi zake vizuri na kuifanya Tanzania kwa nchi Kwanza katika udhibiti wa ubora wa dawa, vifaa, Tiba, vipodozi pamoja na vitendanishi.
WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua maabara ya chakula ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wakati alipotembelea ofisi za Mamlaka hiyo, Mabibo jijini Dar es salam, Machi 6, 2019. Kulia ni Meneja wa Maabara wa TFDA, Danstan Hipolite.
  • Waziri Mkuu Majaliwa aliyasema hayo wakati alipokwenda ziara ya kikazi katika Mamlaka hiyo amesema kuwa katika kufanya udhibiti huo waongeze kituo vya ukaguzi katika mikoa hasa katika mikoa inayopakana na nchi jirani ikiwa kwa ajili ya kulinda afya za watanzania kutokana na mwiingiliano wa dawa na vyakula nchi zilizo jirani kwa kuweza akiingia bila ukaguzi.
  • Amesema kuwa katika kufanya kazi za kisayansi wafanyakazi waongozwe na weledi pasipo na mwanya wa kuwepo kwa rushwa katika ukaguzi wa bidhaa mbalimbali.
WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ameshika dawa ya malaria aina ya DUO -COTECXIN, halisi kulia na bandia kushoto zilizopimwa na kugundulika hivyo katika Maabara ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wakati alipotembelea ofisi za TFDA , Mabibo jijini Dar es salaam, Machi 6, 2019. Wa pili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angela Kairuki na wa tatu kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu., kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa TFDA, Candita Shirima.
  • Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa changamoto rasilimali watu atatue Waziri mwenye dhamana kwa kuomba kibali serikalini katika kuongeza utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja wawekezaji wakati serikali ikiwa katika kipindi cha kuimarisha uchumi. Aidha amesema katika mnyororo wa upimaji wa bidhaa mbalimbali kusiwepo kwa Mahusiano na wataalam na mwenye bidhaa kinachotakiwa kufanyika kwa mfanyabiashara kuacha bidhaa ya kufanyiwa uchunguzi katika mapokezi na iondolewe jina la kampuni.
  • Amesema katika kufanya uchunguzi watalaam lazima wajiridhishe kutokana na bidhaa hizo zinaingia kwa walaji ambao lazima afya zao zilindwe. Nae Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa TFDA inambeba katika majukwaa ya kimataifa katika umahiri wa mfumo wa udhibiti.
WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu upimaji wa dawa na vyakula kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Justin Mkisi (kulia) wakati alipotembela ofisi za Mamlaka hiyo, Mabibo jijini Dar es salaam, Machi 6, 2019. Wa tatu kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angela Kairuki, wa nne kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na wa tano kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Candita Shirima
  • Amesema maagizo ya Waziri Mkuu watayasimamia katika utekelezaji ikiwa ni kuboresha huduma katika Mamlaka hiyo na kuleta matokeo katika uchumi wa viwanda. Kwa upande Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji
  • Angela Kairuki amesema kuwa TFDA katika uwekezaji ni daraja na kutaka watu wenye maamuzi katika kituo vya uwekezaji ili kurahisisha huduma kwa wawekezaji wanaopita (TIC).
Ad

Unaweza kuangalia pia

ONGEZENI KASI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI – DKT. CHAULA

Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma …

Oni moja

  1. Maligisa James Dotto

    Sawa, japo hamjasema Tanzania imekuwa ya kwanza wapi? Barani Africa, Duniani au Africa Mashariki?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *