UMOJA WA ULAYA EU WATOA MAFUNZO YA UDHIBITI WA VYANZO VYA MIONZI KWA NCHI TANO ZA AFRIKA.

  • Umoja wa Ulaya EU umetoa mafunzo ya udhibiti wa uingizaji wa vyanzo vya mionzi kwa nchi tano za Afrika kwa lengo la kusaidia udhibiti  wa uingizaji wa vyanzo vya mionzi bila kufuata utaratibu pamoja na utoroshwaji wa vyanzo vya mionzi vilivyoibiwa kwa matumizi yasiyo salaama na hatarishi.
  • Washiriki  wa mafunzo haya ni kutoka taasisi mbali mbali zikiwemo Mamlaka za Mapato, Forodha na vyombo vya ulinzi na usalama kutoka  katika nchi za Malawi, Rwanda, Kenya, Zambia  na wenyeji Tanzania kupitia  Tume ya Nguvu za Atomiki.
  • Huu ni mwendelezo wa mafunzo kwa nchi za Afrika katika kusaidia kupambana na tabia ya uingizwaji wa vyanzo vya mionzi  ambavyo kwa namna moja ama nyingine hupelekea kuleta madhara  kwa binadamu.
  • Mafunzo hayo yanahusisha mafunzo kwa vitendo ikiwemo utambuzi kwa kutumia vifaa maalumu vilivyopo katika mipaka yote katika nchi hizo  ambapo husaidia kugundua uhalifu wa namna hiyo.
  • Mshiriki wa mafunzo hayo kutoka Tanzania Mhandisi Exavier Zakaria amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia sana hasa kwa wao waliopo katika mipaka amesema wamekuwa wakikutana na masuala mengi ikiwemo baadhi ya wafanyabiashara ambao huenda kinyume na sheria na taratibu zilizowekwa za usafrishaji wa vyanzo vya mionzi.
  • ‘’Ukweli mafunzo yamekuja kwa wakati sahihi  na yatasaidia sana katika kuongeza ujuzi kwenye utambuzi wa vyanzo  vya mionzi ambavyo ni hatarishi kwa binadamu’’ alisema Mhandisi Zakaria
  • Naye mshiriki mwingine wa mafunzo hayo kutoka Tanzania , Bwana Patrick Simpokolwe amesema kuwa kutokana na mbinu za uhalifu za uingizaji wa mionzi isiyo salama katika mipaka mbali mbali katika nchi za Afrika anaamini  mafunzo haya yatamsaidia katika kugundua mbinu mbali mbali za uhalifu na kuweza  kudhibiti.
  • ‘’Tumekuwa tukikumbana na udanganyifu mkubwa kwenye mipaka  kutokana na mbinu mpya zinazotumiwa na wasafirishaji wa bidhaa mbali mbali zikiwemo zenye vyanzo vya mionzi kutoka  na kuingia ndani ya nchi hivyo mafunzo haya yatawezesha kuwabaini wahalifu wa namna hiyo’’ alisema Simpokolwe.
  • Mshiriki mwingine kutokea nchini Kenya Bi Evalyne  Rotich  amesema kuwa kutokana na uwezekanao wa kutokea uhalifu kila wakati na kwamba mafunzo hayo yatawezesha sana kutambua watu ambao sio wema wenye lengo la kupitisha vitu vyenye vyanzo vya mionzi  mipakani ambavyo vinaweza kudhuru wananchi katika nchi husika .
  • ‘’Umakin utaongezeka kwetu kwani mbinu tulizopatiwa zitatuwezesha kutambua vitu vyote ambavyo vitapitishwa bila kufuata utaratibu husika’’ alisema Rotich.
  • Kwa upande wake mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo kutoka umoja wa Ulaya (EU) , Bi Katrijin Vandersteen amesema kuwa katika nchi za Afrika kumekuwa na tatizo la uingizaji wa vyanzo vya mionzi visivyo salama hivyo kwakutolewa  mafunzo hayo kutolewa yataweza  kusaidia katika uimarishaji wa utambuzi  na udhibiti  katika maeneo ya mipaka kwenye nchi mbali mbali.
  •  ‘’Tunaamini kuwa washiriki hawa watapata  uelewa  zaidi juu ya utambuzi wa vyanzo vya mionzi visivyo salama kwa lengo la kusaidia kutoleta madhara kwa binadamu kwenye nchi husika na dunia kwa ujumla mara baada ya kukamilika  kwa mafunzo haya ’’ alisema Vandersteen.
  • Mfunzo haya yanafanyika katika Makao Makuu ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, jijini Arusha kuanzia tarehe 4 hadi 8 Machi 2019.
Ad

Unaweza kuangalia pia

KINONDONI YA TUMIA BILIONI 1.5 UJENZI WA MADARASA YA SHULE ZA MSINGI

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imetumia kiasi cha shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *