Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (mbele) akiwaongoza viongozi wa Wilaya ya Uyui na wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora -Uyui kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo leo. Picha na Tiganya Vincent

UJENZI WA HOSPTALI YA WILAYA YA UYUI MKOANI TABORA WATAKIWA KUKAMILIKA JUNI MWAKA HUU

WAZIRI JAFO
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (katikati) akitoa maagizo kwa viongozi wa Wilaya ya Uyui na wa Hamashauri ya Wilaya ya Tabora -Uyui baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo
  • Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora(UYUI) umeagizwa kuongeza kasi katika ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ili ifikapo Juni mwishoni mwaka huu majengo yote  waliyopangiwa yamewe yamekamilika.
  • Agizo hilo limetolewa  wilayani Uyui na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi huo.
WAZIRI JAFO
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (katikati) akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya ( wa pili kutoka kulia) kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo
  • Alisema fedha zipo hakuna sababu ya kazi ya ujenzi kwenda pole pole kwa kuwa wananchi wanasubiri huduma hiyo kwa hamu.
  • Jafo alisema katika Halmashauri nyingine ambapo walipewa fedha pamoja tayari majengo yao yako usawa wa madirisha lakini ya Uyui bado yako katika ngazi za msingi.
  • Alisema sio vizuri kutumia fundi mmoja kujenga majengo yote ni vema wakatumia mafundi wengi ili kuharakisha kazi ya ujenzi wa Hospitali hiyo.

WAZIRI JAFO

  • Aidha Waziri huyo alisema ni jambo la kusikitishwa kuona Halmashauri hiyo imetumia kiasi cha milioni 8 kusafisha eneo badala ya kuwahamisha wananchi kushiriki katika usafishaji wa ili fedha hizo zisaidie ujenzi.
  • Alisema fedha walizozitumia katika usafishaji wa eneo zingeweza kusaidia katika uendeleza wa ujenzi wa majengo hayo kama wananchi wangeshiriki katika usafishaji wa eneo badala ya kukodi Greda na kulipa kiasi hicho cha fedha.
  • Naye Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya alimwakikishia Waziri kuwa watajitahidi kukamilisha majengo hayo katika kipindi kilichopangwa na kwa kuzingatia maelekezo ya TAMISEMI ili fedha zitakazobaki zisaidie kujenga kichoma taka.
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI UMMY AWATAKA WAZAZI KUWEKEZA KATIKA AFYA ZA WATOTO

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka wazazi kuwekeza …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *