UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA BAHI WAFIKIA ASILIMIA 87.6 KUKAMILIKA

 • Mkuu wa Mkoa wa Dodoma dokta Bilinith Mahenge amepongeza kasi na mshikamano uliotumika katika kujenga Hospitali ya Wilaya ya Bahi ambayo ujenzi wake umefikia wastani wa asilimia 87.6.
 • Pongezi hizo amezitoa wilayani humo baada ya kushuhudia majengo saba ya hospitali hiyo yakiwa katika hatua ya mwisho kukamilika kutokana na mshikamano uliopo baina ya viongozi wa wilaya, mkandarasi na wananchi wa wilaya hiyo.
DD 2-01
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akikagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Bahi akiwa ameambatana na mkuu wa wilaya hiyo Mwanahamisi Munkunda, mwenyekiti wa halmashauri Danford Chisomi, Mkurugenzi wa halmashauri Dokta Fatuma Mganga na mganga mkuu wa wilaya Dokta Philipina Philipo.
 • Akizungumza baada ya kukagua ujenzi huo dokta Mahenge amesema mwezi februari alitembelea eneo hilo na ujenzi ulikuwa haujaanza lakini ndani ya miezi nne hospitali imejengwa na ipo katika hatua za mwisho kukamilika.
 • “Mwezi februari nilikuja hapa nilikuta kamanda mmoja anafyatua tofali lakini ndani ya miezi minne majengo yamesimama, nawapongeza sana, najua ushirikiano wenu ndio umewafikisha hapa,”alisema dokta Mahenge.
DD 3-01
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akikagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Bahi akiwa ameambatana na mkuu wa wilaya hiyo Mwanahamisi Munkunda, mwenyekiti wa halmashauri Danford Chisomi, Mkurugenzi wa halmashauri Dokta Fatuma Mganga na mganga mkuu wa wilaya Dokta Philipina Philipo.
 • Amezitaka halmashauri nyingine mkoani humo zinazojenga hospitali hizo kuiga mfano wa halmashauri hiyo ambayo imeonyesha ushirikiano baina yao wenyewe na ushirikiano baina yao na wananchi.
 • Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda amesema katika kufanikisha ujenzi huo wananchi wamechangia nguvu zao, watendaji wa idara wameshindanishwa katika kusimamia na mkandarasi kujenga.
DD 4-01
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akikagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Bahi akiwa ameambatana na mkuu wa wilaya hiyo Mwanahamisi Munkunda, mwenyekiti wa halmashauri Danford Chisomi, Mkurugenzi wa halmashauri Dokta Fatuma Mganga na mganga mkuu wa wilaya Dokta Philipina Philipo.
 • “Ujenzi wetu huu kwa kiasi kikubwa tumeshirikisha wananchi, na hata hapa wananchi tumewaganya kwa kila jengo kwa ajili ya kufanya usafi, na wakuu wangu wa idara kila mtu tulimkabidhi jengo lake asimamie hivyo walikuwa wanashindana hapa,”alisema mkuu wa wilaya huyo.
 • Amesema katika ujenzi wa majengo saba, jengo la utawala limefikia asilimia 89, Wagonjwa wa Nje 89, Maabara 89, Jengo la kufulia 89, jengo la kutunzia dawa 89 jengo la mionzi 89 na jengo la mama na mtoto 79.
DD 4-01
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akikagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Bahi akiwa ameambatana na mkuu wa wilaya hiyo Mwanahamisi Munkunda, mwenyekiti wa halmashauri Danford Chisomi, Mkurugenzi wa halmashauri Dokta Fatuma Mganga na mganga mkuu wa wilaya Dokta Philipina Philipo.
 • Mwananchi Amina Jumaa amesema, kujengwa kwa hospitali hiyo kutapunguza adha za kutembelea umbeli mrefu, kutumia rasilimali fedha na rasilimali nyingine kwenda hospitali ya Rufaa ya Dodoma.
 • “Tunaishukuru serikali yetu kwa kutujali, hospitali hii ikikamilika itatusaidia sana hasa sisi akina mama, tukitaka kujifungua kama tulikuwa tunaenda Dodoma mjini na kutoka kijijini mpaka huko karibu kilomita 60, lakini hospitali hii ikikamilika tutajifungulia hapa na hivyo kupunguza vifo vya akina mama na watoto, “alisema mama huyo.
DD 5-01
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akikagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Bahi akiwa ameambatana na mkuu wa wilaya hiyo Mwanahamisi Munkunda, mwenyekiti wa halmashauri Danford Chisomi, Mkurugenzi wa halmashauri Dokta Fatuma Mganga na mganga mkuu wa wilaya Dokta Philipina Philipo.
 • Hospitali ya Wilaya ya Bahi ni miongoni mwa hospitali 67 zinazojengwa katika wilaya mbalimbali nchini lengo likiwa kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI UMMY AWATAKA WAZAZI KUWEKEZA KATIKA AFYA ZA WATOTO

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka wazazi kuwekeza …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *