Maktaba ya Mwezi: June 2020

TANZANIA YAFANIKIWA KUPUNGUZA UINGIZAJI WA DAWA ZA KULEVYA NCHINI KWA 90%

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO Tanzania imefanikiwa kupunguza uingizaji wa dawa za kulevya kwa asilimia 90 kufuatia jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali za  kupunguza tatizo la dawa za kulevya nchini. Akizungumza leo jijini Dodoma, katika Maadhimisho ya Siku ya Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya …

Soma zaidi »

UJENZI WA BARABARA YA TABORA – KOGA – MPANDA KM 324.7 KWA KIWANGO CHA LAMI WAFIKIA ASIMILIA 48

Kazi za ujenzi wa tabaka la juu la lami ukiendelea katika barabara ya Tabora – Koga – Mpanda (km 342.7); sehemu ya Usesula – Komanga, mkoani Tabora. Kazi za kusambaza lami katika sehemu ya barabara ya Komanga – Kasinde ikiendelea. Kazi hiyo inafanywa na mtambo maalum wa kisasa unaogusa upana …

Soma zaidi »

WAZIRI LUKUVI AAGIZA WASAJILI WASAIDIZI WA HATI OFISI ZA ARDHI ZA MIKOA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

Na Munir Shemweta, WANMM SINGIDA Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewataka Wasajili WasaidIzi wa Hati kwenye Ofisi za Ardhi za Mikoa kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na faida ya ofisi ya Msajili wa Hati. Akizungumza wakati wa kuzindua ofisi ya ardhi ya mkoa wa Singida …

Soma zaidi »

MAELEKEZO YA ULIPAJI WA ADA ZA SHULE ZISIZO ZA SERIKALI BAADA YA JANGA LA CORONA

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inapenda kutoa maelekezo kufuatia malalamiko kuhusu ulipaji wa ada na malipo mengine kwa shule za Msingi na Sekondari zisizo za Serikali zitakapofunguliwa baada ya janga la Corona. Wizara inaelekeza na kusisitiza kuwa wanafunzi wote wapokelewe kwa ajili ya kuendelea na masomo ifikapo tarehe 29/06/2020. …

Soma zaidi »

PROF. KABUDI AKUTANA, KUMUAGA BALOZI WA IRELAND NCHINI TANZANIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi, amekutana na kumuaga Balozi wa Ireland nchini, Paul Sherlock ambaye amemaliza muda wake wa utumishi na amemtakia maisha mema na kumwambia kuwa ni matarajio yake kuwa atakuwa balozi mwema kwa Tanzania nchini Ireland na kwingineko duniani. …

Soma zaidi »

MKUTANO WA MAWAZIRI WA KAMATI YA SADC YA ASASI YA USHIRIKIANO WA SIASA, ULINZI NA USALAMA KWA NGAZI YA MAKATIBU WAKUU WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Mkutano wa Mawaziri wa Kamati ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ya Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama kwa ngazi ya Makatibu Wakuu/ Maafisa Waandamizi umefanyika tarehe 25 Juni,2020, Jijini Dar es Salaam kwa njia ya Mtandao (Video Conferencing). Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama …

Soma zaidi »

TAMISEMI YARIDHISHWA NA MATUMIZI MAZURI YA FEDHA ZA MAPATO YA NDANI KATIKA MIRADI YA MAENDELEO MANISPAA YA KINONDONI

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Josephat Kandege ameridhishwa na matumizi ya fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri  zilizotumika katika utekelezaji wa miradi ya maedeleo iliyokamilika kwa wakati na viwango. Amesema kuwa Manispaa hiyo ni mfano wakuigwa kwa kuwa …

Soma zaidi »

TANZANIA YAENDELEA KUZIOMBA TAASISI ZA FEDHA ZA KIMATAIFA KUSAMEHE MADENI NCHI ZINAZOENDELEA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuziomba taasisi za fedha za kimataifa pamoja na nchi za Jumuiya ya madola kufikiria kufuta kabisa madeni yaliyokopeshwa kwa nchi zinazoendelea ili fedha hizo ziweze kutumika kupambana na athari zilizotokana na Covid 19. Ombi hilo limetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje …

Soma zaidi »