DR. DUGANGE AWATAKA TARURA KUSIMAMIA MIKATABA

Nteghenjwa Hosseah, OR- TAMISEMI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Dk Festo Dugange ameutaka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha mikataba ya ujenzi wa barabara inazingatia masharti na miradi inatekelezwa kwa wakati.

Dk. Dugange aliyasema hayo jijini hapa alipokwenda kukutana na uongozi wa TARURA kwa madhumuni ya kujitambulisha, kutathimini kwa pamoja na kukubaliana njia ambayo inapaswa kufuatwa katika kutekeleza wa miradi ya barabara vijijini na mijini.

Alisema ni vyema mikataba yote ya ujenzi wa barabara ikazingatia masharti yaliyopo kwenye mikataba hivyo kuondoa changamoto ya kutotekelezwa kwa wakati.

“ Mara nyingi kumekuwa na changamoto ya mikataba kutotekelezwa kwa wakati, mikataba inasainiwa haimaliziki kwa wakati tunalazimika kuongeza muda wa utekelezaji wake jambo ambalo linaongeza gharama, kupunguza thamani za fedha na kupunguza ufanisi wa malengo ya serikali.”

“ Tumekubaliana kwamba TARURA tumepewa sekta nyeti ya kuchangia uchumi katika nchi yetu, wananchi wanahitaji kujijenga kiuchumi kwa kusafirisha bidhaa zao, mazao ya kilimo biashara na huduma mbalimbali za kijamii.”

Ad
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Dk Festo Dugange

Aidha, Dk Ndugange alitoa rai kwa makandarasi watakaopata kazi za TARURA kuhakikisha wanazingatia mikataba yao na kusisitiza kuwa Serikali haitakuwa tayari kuona mikataba inapita muda wake wa utekelezaji.

“ Pia thamani ya fedha katika miradi ya barabara lazima izingatiwe, tunapenda kuona fedha zinazopelekwa kwenye matanegezo na ujenzi wa barabara zetu inaonesha thamani yake na barabara zinajengwa kwa ufanisi na zinadumu.”

Dk Dugange pia aliitaka TARURA kuwa na malengo ya kila mwaka na kubainisha barabara ngapi zinajengwa kutoka ngazi ya changarawe kwenda lami na kutoka za udogo kwenda changarawe.

Pia ameutaka Wakala huyo kuhakikisha inazingatia suala la matengenezo ya mara kwa mara na kuzingatia tahamani ya fedha na kufanyika kwa wakati ili kuondoa usumbufu kwa wananchi.

Aidha, Dk Ndugange aliipongeza TARURA kwa utengenezaji wa barabara kwani utendaji kazi kasi imeongezeka lakini pia ufanisi na thamani ya fedha katika ujenzi wa barabara umeongezeka.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Askofu Dkt Maasa OleGabriel RAIS SAMIA ANATEKELEZA MAAGIZO YA MUNGU YA KUITUNZA BUSTANI YA EDENI

Askofu Dkt. Maasa OleGabriel Katibu Mkuu Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania na Askofu wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *