WAITARA ATETA NA WAFANYABIASHARA CHUMA CHAKAVU, ARIDHISHWA KIWANDA CHA KUREJELEZA CHUPA ZA PLASTIKI

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Mwita Waitara akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara wa chuma chakavu wa jijini Mwanza aliofanya kikao nao kwa lengo la kusikiliza changamoto zao na kutoa elimu ya utaratibu wa vibali.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Mwita Waitara amewataka wafanyabiashara wa chuma chakavu kuwa waaminifu na kuepuka kujihusisha kuhujumu miundombinu.

Waitara ametoa kauli hiyo leo Desemba 22, 2020 alipofanya kikao na wafanyabiashara hao jijini Mwanza ambapo alionya pamoja na Serikali kuitambua biashara hiyo lakini wapo baadhi ya watu wanaharibu miundombinu na kuwauzia kama chuma chakavu kinyume cha sheria.

Ad
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Mwita Waitara akipata maelezo kuhusu shughuli za kiwanda cha kurejeleza chupa za plastiki cha Falcon jijini Mwanza kutoka kwa Meneja Uendeshaji Rajat Gupta alipofanya ziara kiwandani hapo.

Aliwataka wafanyabiashara hao kufanya kazi na Serikali katika kuwafichua wanaoharibu miundombinu kisha kuwauzia kama vyuma chakavu kwani kitendo hicho ni sawa na uhujumu uchumi na wanachafua jina lenu.

“Ukifanya kazi kwa mujibu wa sheria hautagombana na mtu yeyote wa Serikali, umepewa kibali cha kununua chuma chakavu kiwe chakavu kweli na anayekuuzia lazima umfahamu ili tukifuatilia tusikupe mzigo huo na mjua kabisa hili ni jambo baya na kuna wenzenu walikamatwa na wapo katika hatua za kuwajibishwa,” alionya.

Aidha, Naibu waziri aliongeza ipo haja ya kumshauri Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais ambaye ndiye mwenye dhamana ya vibali tupitie upya vibali hivyo na ikibainika wafutiwe akisema kuwa ni kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Mwita Waitara (katikati) akiwa amekali kiti na kusaini kitabu cha wageni juu ya meza vyote vilivyotengenezwa kwa chupa za plastiki zilizorejelezwa alipotembelea kiwanda cha Falcon cha jijini Mwanza.

Awali akitembelea kiwanda cha kurejeleza chupa za plastiki cha Falcon jijini Mwanza alipongeza jitihada za mwekezaji huyo kwa kusaidia kusafisha mazingira kwa kukusanya chupa hizo.

“Naomba niwapongeze sana kwani tutakumbuka tarehe moja Juni wakati tulipopiga marufuku mifuko ya plastiki mzigo wa tani takriban nane ulisalimishwa.

“Mnasaidia sana kusafisha mazingira na mnatoa ajira maana yake wananchi wakikusanya chupoa hizi wanapata chochote ni ajira hii na nimefurishwa sana mnazalisha product zingine naona benchi haoa meza badala ya kukata miti na kuharibu mazingira,” alisema.

Naibu Wazitri Waitara yupo katika ziara mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa lengo la kutoa elimu kuhusu utunzaji wa mazingira akiambatana watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). 

Ad

Unaweza kuangalia pia

Uzinduzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya UCSAF Dodoma: Kuimarisha Mawasiliano Vijijini

25 Aprili 2024, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *