UJENZI WA BARABARA ZA KIWANGO CHA LAMI KATIKA MJI WA SERIKALI

Ujenzi wa barabara za kiwango cha lami katika mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma wenye gharama ya bilioni 88.1 na urefu wa kilomita 51.2 umefikia asilimia 56.


 
Hayo yamesemwa na Katibu wa kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na Uratibu wa ujenzi wa mji wa Serikali, Meshack Bandawe wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hizo jijini Dodoma.

Ad

“Sasahivi kinachoendelea ni ujenzi wa barabara za lami zinazozunguka ndani ya mji wa Serikali na ujenzi huu umefikia sehemu nzuri na ikifika Julai mwaka huu utakuwa umekamilika”, aliongeza Bw.Bandawe

Aidha amesema ujenzi huo unahusisha ujenzi wa barabara za njia mbili za urefu wa kilomita 22.4 na zile zenye njia moja zenye urefu wa kilomita 28.8,pamoja na ujenzi wa miundombinu mingine kama maji, umeme,gesi,tehama mawasiliano,zimamoto na uokoaji,maduka makubwa pamoja na huduma za treni nk.
 
Katika hatua nyingine amesema ujenzi wa majengo marefu ya wizara awamu ya pili utaanza mara baada ya taratibu za kimamlaka na idhini kukamilika.

Mradi wa ujenzi wa barabara za mji wa serikali mtumba unatekelezwa na mkandarasi China heinan international cooperation co. Ltd (chico) na Unasimamiwa na wakala wa barabara za vijijini na mijini (Tarura), ulizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli mwezi Machi 2019.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Serikali ya Tanzania na Czech Zakubaliana Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili

Serikali za Tanzania na Czech kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kuvutia uwekezaji kati yao. Kuondoa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *