WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AMEWATAKA WATUMISHI WA TBS NA WMA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe wakuwa wameambatana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya wakipokea maelezo kutoka Mkuu wa maabara ya kemia, Florian Bataganwa wakati wakikagua maabara za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Januari 11, 2021 walipofika katika makao makuu ya TBS yaliyopo ubungo – Dar es salaam.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe  amewataka watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Wakala wa Vipimo (WMA) kufanya kazi kwa uadilifu, weledi  na kuwafikiria wafanya biashara wakati wakitoa huduma kwa wafanyabiashara ili kuendelea kutengeneza taswira nzuri ya bidhaa  za Tanzania katika soko la ndani nan je ya nchi.

Waziri Mwambe aliyasema hayo alipokuwa akiongea na menejimenti na wafanyakazi wa TBS na WMA alipofanya ziara katika  taasisi hizo akiambatana na Naibu Waziri wa Viwanda Exaud Kigahe pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa Wizara ya Viwanda na Biashara tarehe 11 Januari 2021 katika taasisi husika.

Ad
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe (katikati) na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara akiongea na wafanyakazi wa Shirika ya Viwango Tanzania (TBS) ikiwa ni kikao cha kwanza na Taasisi hiyo tangu kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara hiyo, ubungo – Dar es salaam. Januari 11, 2021

Akiwa TBS, Waziri Mwambe ameiagiza TBS kufanya ukaguzi wa bidhaa kwa kushirikiana na taasisi nyingine  zinazohusika na ukaguzi wa mizigo bandarini  na mipakani ili kupunguza muda unatumika kugagua bidhaa hizo,kupunguza mianya ya rushwa na kurahisisha utoaji wa mizigo hiyo kwa haraka.

Aidha, Mhe. Waziri aliitaka TBS kupunguza muda wa kuandaa viwango kutoka miezi 9 hadi miezi 3 na muda wa usajili wa bidhaa na kutoa alama ya ubora kutoka miezi 3 hadi mwezi mmoja ili kuwarahisishia wajasiliamali kuwezakufanya na kukuguza biashara zao kwa urahisi.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe akiwa kwenye kikao na Bodi, menejimenti na uongozi wa Taasisi ya Wakala wa Vipimo Tanzania Dar es salaam, Januari 11, 2021

Vilevile Mhe. Waziri ameielekeza TBS kufanya kazi kwa pamoja na Shirika la Kuhudumia Viwand Vidogo (SIDO)  na  Balaza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC katika kuandaa Viwango na miongozo yenye vigezo rahisi vitakavyowawezesha wajasiliamali kuanzisha viwanda vidogo  majumbani ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa,kukuza biashara kuongeza ajira nakuongeza pato la taifa.

Mwambe pia ameihimiza  TBS kufanya kazi kwa karibu na Maafisa Biashara wa Halmashauri ili kurahisisha utoaji wa elimu na usimamizi wa viwango kwa wajasiliamali  ili kupanua uwigo wa utoaji huduma na kuwafikia wajasiliamali wengi walioko katika halmashauri hizo.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akiwa katika picha ya pamopja na Bodi, menejimenti, uongozi na wafanyakazi wa Taasisi ya Wakala wa Vipimo Tanzania Dar es salaam, Januari 11, 2021

Naye Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amezitaka TBS na WMA kuhakikisha zinasimamia viwango na ubora pamoja na vipimo sahihi vya bidhaa za Tanzania ili kuziwezesha bidhaa hizo kuingia katika soko la ushindani ndani na nje ya nchi kwa ufanisi.

Aidha naibu Waziri aliziagiza taasisi hizo kuendelea kuimarisha ukaguzi wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi zinakuwa na viwango navipimo sahihi ili kuiepusha Tanzania kuwa dampo la bidhaa hafifu.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Mitazamo ya Uongozi ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu katika Sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii, na Haki za Watoto

Ummy Ally Mwalimu ameonyesha mitazamo ya uongozi yenye mwelekeo wa kujali maendeleo na ustawi katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *