Ni Mkurugenzi wa Shirika la kimataifa la nguvu ya Atomiki duniani kanda y Afrika Profesa Shaukat Abdulrazak(Kulia ) akipeana mkono na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh Simai Mohamed Mara baada ya Kufanya Mazungumzo yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kushirikiana baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Shirika hilo

ZANZIBAR KUTOA USHIRIKIANO KWA SHIRIKA LA NGUVU ZA ATOMIKI DUNIANI

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Simai Mohamed Said amesema Zanzibar itaendelea kutoa ushirikiano kwa shirika la nguvu za atomiki Dunia  ili kukuza na kuimarisha teknolojia ya utumiaji wa mionzi.

MKURUGENZI
Mkurugenzi wa Shirika la kimataifa la nguvu ya Atomiki duniani kanda y Afrika Profesa Shaukat Abdulraza akizungumza katika mkutano  wenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kushirikiana baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Shirika hilo
  • Ameyasema hayo katika mkutano wa pamoja na ujumbe wa shirika la Nguvu za Atomic Duniani (IAEA) kanda ya Afrika, Simai amesema Zanzibar Bado ipo chini kwa utumiaji wa Teknolojia ya mionzi.
  • Aidha ameutaka ujumbe huo kuunganisha nguvu na Wizara ya Elimu kupitia chuo cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ili nao waweze kutoa Elimu kuhusiana na matumizi ya Teknolojia ya mionzi.
  • Nae Mkurugenzi wa shirika la nguvu za atomic Duniani (IAEA) kanda ya Afrika Profesa Shaukati Abdulrazak amesema malengo hasa ya IAEA ni kutumia Teknolojia katika uzalishaji wa vyakula, kuondoa wadudu waharibifu wa mazao na kupambana na maradhi ya saratani.
  • Aidha amesema shirika la IAEA lipo tayari kuwajengea uwezo wazanzibar ili waweze kutumia Teknolojia kwa lengo la kuleta maendeleo zaidi.
M
Baadhi ya washiriki wakifatilia kinachoendelea kwenye mkutano
  • Pia amesema Teknolojia hiyo ni kuhakikisha kila chakula ni salama kwa matumizi ya kibinaadam.
  • Alisema wataendeleza ushirikkano ili kuhakikisha Zanzibar nayo inapata kifaa cha kupimia maradhi ya saratani.
  • Nae Mkurugenzi mkuu wa tume ya Nguvu za Atomic Tanzania (TAEC) Profesa Lazaro Busagala amesema kwa kazi ya majaribio ya mwanzo ya shirika hilo la Zanzibar ni kuhakikisha hakuna kabisa wadudu wa Mbung’o, zoezi ambalo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
  • Aidha amesema ushirikiano mzuri ndio utakaoosababisha wazanzibar kuendelea mbele kiteknolojia.
Ad

Unaweza kuangalia pia

MWANAFUNZI WA MALANGALI AINGIA KUMI BORA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

#SisiTumeona SISI WATANZANIA TUNAWEZA Hivi sasa watoto wetu wanapata elimu bure bila malipo! ——————————— Matokeo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *