Mhe. ANTONY MTAKA Ni nani? Historia yake hii hapa.

“Nimeuliza ripoti ya Wakuu wa Mikoa Tanzania wanaofanya vizuri, wakaniletea ANTHONY MTAKA ndiye Namba Moja, na Namba Mbili ni yeye. Kwa kifupi hana mfano”

Mh. Rais Dr. JPM, Simiyu.

Ad

Je ni nani huyu Mkuu wa Mkoa Mhe. MTAKA.. na ametokea wapi? Mheshimiwa MTAKA anajipambanua katika sifa zifuatazo:-

1. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mheshimiwa ANTHONY JOHN MTAKA CHIGANGA alizaliwa tarehe 5 Julai 1983 mkoani Mara. Yeye ni mtoto wa kwanza kati ya wanne wa Bi. Merciana Mageti na Bw. JOHN MTAKA CHIGANGA.

2. Mheshimiwa MTAKA alisoma Shule ya Msingi Suguti, Musoma mkoani Mara ambapo alimaliza mwaka 1996.

3. Mheshimiwa MTAKA alisoma Shule ya Sekondari ya Mwembeni, Musoma mkoani mara toka mwaka 1997 hadi 2000 na akasoma kidato cha tano na sita mwaka 2001 hadi 2003 huko Kilimanjaro.

4. Mwaka 2004 alijiunga na Chuo cha Ualimu Marangu lakini akaacha baada ya nusu mhula na kujiunga mafunzo ya Jeshi la polisi kabla ya kujiunga ambapo yeye ni F.6886 PC A. MTAKA. Baadae mheshimiwa MTAKA akaenda kusoma Chuo Kikuu Mzumbe alikopata shahada ya Utawala mwaka 2009.

5. Mheshimiwa MTAKA aliteuliwa na Rais DR. JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu tarehe 13 Machi 2016.

6. Akiwa sasa na umri wa miaka 35, Mheshimiwa MTAKA ni mmoja wa Wakuu wa mikoa wadogo kabisa kuwahi kutokea nchini.

7. Kabla ya kuwa Mkuu wa mkoa Mheshimiwa MTAKA alihudumu PPF, pia alikuwa Mkuu wa Wilaya za Mvomero na Hai baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa JAKAYA KIKWETE, Rais wa awamu ya nne wa nchi yetu.

8. Mheshimiwa MTAKA ana vipaji lukuki: ni mwanariadha na Mwenyekiti wa chama cha riadha nchini, ni askari, ni mwimbaji hodari wa nyimbo za injili na ametunga nyimbo zake na karibuni atazirekedi, ni mwandishi mzuri wa makala, ni msomaji mzuri wa vitabu vya Kiswahili na Kiingereza na pia ni mpenzi kindakindaki na mwanachama wa YANGA, ambayo kihistoria, ni moja ya timu bora kuliko zote zilizowahi kutokea nchini.

9. Mheshimiwa MTAKA ni Kiongozi Mnyenyekevu, mwenye busara na staha na asiye na mihemko. Ni aina ya viongozi wa kisasa mwenye hofu ya Mungu na aliye na heshima kwa wakubwa na wadogo.

10. Mheshimiwa MTAKA sio mpenda ‘kiki’ au sifa za kijinga. Ni mwerevu, mwenye kuamini umoja katika kuleta maendeleo na kuwa uongozi si bla bla na kupandisha mabega juu bali ni kwaajili ya kuwatumikia wananchi . Aliwahi kuandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa, (namnukuu) “Niwakumbushe tu wenzangu kuwa cheo ni dhamana. Walikuwepo viongozi kabla yetu na watakuja wengine baada yetu. Mkipewa uongozi epukeni kubeba hivi vyeo mabegani” (Mwisho wa kunukuu)

11. Mheshimiwa MTAKA ni mchapakazi hodari. Mkoa wa Simiyu ulianzishwa mwaka 2012 na ulikuwa uko nyuma sana kimaendeleo. Lakini, wakati mikoa mingine mingi bado haisomeki (ikisua sua kimikakati ya maendeleo), mkoa wa Simiyu chini ya uongozi imara wa mheshimiwa MTAKA umepiga hatua kubwa na kuwa mkoa wa kupigiwa mfano. Sherehe za Nane nane kitaifa ambazo mwaka huu zilifanyika Simiyu zilithibitisha hili.

12. Mheshimiwa MTAKA amekuwa na mafanikio katika kuunga mkono azma ya Rais ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati. Mheshimiwa MTAKA ameasisi kauli mbiu aliyojifunza toka Japan : ‘Kijiji Kimoja, Bidhaa Moja’, inayochagiza ujenzi wa viwanda. Tayari Mheshimiwa MTAKA alizindua kiwanda cha maziwa na cha chaki alivyovizindua Novemba 2016 na vingine vipo njiani.

13. Mkoa wa Simiyu umeweza kupata wawekezaji wazawa wengi kutokana na juhudi za Mheshimiwa MTAKA.

14. Mheshimiwa MTAKA ni kipenzi cha wananchi wa Simiyu kutokana na mabadiliko makubwa aliyoyaleta mkoani humo.

15. Mheshimiwa MTAKA amekuwa mstari wa mbele kuhimiza elimu ambapo ameahidi kutoa mamilioni kwa wanafunzi watakaofanya vizuri kitaifa. Aidha, amewaasa wanafunzi hao wasome hadi usiku wa manane ili wafaulu na kuja kuusaidia mkoa wao kupata maendeleo.

16. Mheshimiwa MTAKA alipiga marufuku muhemko usio na kichwa wala miguu wa ma-DC kuwasweka ndani watumishi wa umma ambapo alisema, ” Sisi viongozi tuwalinde watumishi wetu. Nilipoteuliwa kuwa RC niliwajulisha ma-DC wangu kuwa moja ya mambo nisiyotaka kusikia ni watumishi kuswekwa ndani. Sitaki kusikia hata wabunge, madiwani kuswekwa ndani hovyo”.

Kauli hii mujarabu iliungwa mkono na wapenda demokrasia nchini pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Mheshimiwa Joseph Mbilinyi almaarufu kama SUGU, mbunge wa Mbeya mjini ambaye aliyesema,

“Nampongeza sana Mheshimiwa MTAKA. Hawa ndio viongozi wanaopaswa kumsaidia Mheshimiwa Rais. Watendaji wote yaani Mawaziri, ma-RC, ma-DC wawe kama Mheshimiwa MTAKA”.

17. Tarehe 07 Septemba 2017, Mheshimiwa MTAKA alipewa Tuzo na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania kutokana na maendeleo makubwa aliyoyafanya mkoani humo katika kipindi kifupi tu cha uongozi wake ‘Chema Chajiuza, Kibaya Chajitembeza’.

PONGEZI KWA MKUU WA MKOA WA SIMIYU; ENDELEA KUCHAPA KAZI!

Wakuu wa Mikoa na viongozi wengine mnapaswa kujifunza toka kwake kwa kuwa wanyenyekevu, wenye kufuata Katiba, Sheria, Kanuni na Taratibu huku wakitambua kuwa Cheo ni Dhamana na wchape kazi na kuwa wabunifu ili kumsaidie Mheshimiwa Rais katika kufikia azma yake ya kuifanya Tanzania kuwa Donor country!

maana #SisiNiTanzaniaMpyA+

#MATAGA

Tazama video ifuatayo ambayo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akioongeza utendaji kazi na ufanisi wa uongozi wa mkoa wa Simiyu.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KATIBU MTENDAJI SADC, BALOZI WA EU NA BALOZI WA CHINA

Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Februari, 2020 amekutana na Katibu Mtendaji wa …

3 Maoni

  1. Kwa niaba nimpongeze sana Mhe, mkuu wa mkoa wa simiyu kwakweli umeutendea haki uteuzi wako na kurudisha matumaini kwa umma wa Watanzania na kwa Mhe. Rais, kuwa vijana tunaweza. Hongera sana RC simiyu #ipende na kuitumikia inchi yako #Tanzania Mungu mbariki Mhe. Mtaka Mungu ibariki Tanzania.

  2. Binafsi nimpongeze Sana kiongozi huyu ndugu comrade Antony Mtaka kwa haiba nzuri aliyonayo ya kiuongozi.

    Ni wachache Sana Katika karne hii watu hurka yake. Vijana tunapaswa kujifunza mema yake na kuyaishi kwa ajili ya kutujenga katika kutumikia watu.

  3. Inatia moyo kupata kiongozi angalau mmoja (kijana) ambaye ataambukiza wenzake katika uungwana, ujuzi, kufikiri na kuongoza. Vijana wengi hawana staha na ni wepesi kutaka magari , vyeo, ushindi bila kufanya kazi ya kufikiri vizuri na kutoelewa dhana ya maendeleo na uongozi. Mh.Mtaka awape darasa ,pia wateule wafanye mtihani kabla ya kupewa nafasi za uongozi ili kupunguza utumbuaji wa Mh.Rais.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.