KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI: Jukumu la Kiongozi ni kuwatumikia wananchi na si kuweka mbele masĺahi binafsi.

KIJAZI-4.png

KATIBU MKUU KIONGOZI, MHE. MHANDISI BALOZI JOHN KIJAZI katika kikao na Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu, amewataka watendaji hao muhimu wa serikali kuzingatia na kulinda maslahi ya wananchi na si vinginevyo.

Balozi Kijazi alisema;

Ad

“Kauli mbiu ya Kikao Kazi hiki ni Uongozi makini na wapamoja unaozingatia uzalendo, uwajibikaji,utawala Bora na kusimamia kikamilifu rasilimali zetu ni nyenzo muhimu katika kufikisha Tanzania katika uchumi wa Kati.”

“Napenda Kusisitiza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuyafanyia kazi maazimio yote ya Kikao Kazi hiki.”

“Kila Kiongozi afanye kazi kwa kuzingatia dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano inayosisitiza utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea.”

“Kila Kiongozi lazima awe mbunifu katika kutatua changamoto zilizopo katika eneo lake kwa maslahi ya Taifa.”

“Moja ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano ni Kutungwa kwa Sheria mpya za kulinda rasilimali za Taifa letu.”

“Jukumu ĺa Kiongozi ni kuwatumikia wananchi na si kuweka mbele masĺahi binafsi.”

“Kila Kiongozi azingatie Sheria, Kanuni na taratibu ili kufikia malengo ya kujenga uchumi wa Viwanda kwa wakati.”

“Kikao Kazi hiki kinalenga kubadilishana uzoefu, kuibua changamoto na kuweka mikakati ya kuzitatua.”

KIJAZI-2.png

“Mifumo tuliyoifanyia mabadiliko ni pamoja na miundo ya Wizara zote iliyoanza kutumika mwezi Julai 2018 ikilenga kuondoa changamoto zilizokuwepo awali ikiwemo kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.”

“Makatibu Wakuu hakikisheni mnasimamia utekelezaji wa majukumu yenu kwa kuzingatia miundo mipya ya Wizara iliyopitishwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.”

“Serikali inaendelea kupitia miundo ya Taasisi zake na kuifanyia marekebisho ili iendane na matakwa ya Serikali ya Awamu ya Tano.”

“Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa Kinafanyika kwa siku tatu Jijini Dodoma.”

“Ni imani yangu kuwa washiriki wote mtanufaika na mada zitakazowasilishwa ikiwa ni pamoja na Mawasiĺiano ya Serikali kwa umma.”

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AMUWAKILISHA RAIS DKT. MAGUFULI MKUTANO WA AALCO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *