MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKURUGENZI MKAZI WA AfDB NA MABALOZI WAWILI LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Dkt. Alex Mubiru ambaye alifika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha.

Makamu wa Rais amesema kuwa AfDB imeahidi kuendelea kushirikiana na kuisaidia Tanzania kutokana na hatua kubwa ya kimaendeleo ambayo nchi yetu imeonyesha.

Ad

Pamoja na mambo mengine Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika alisema kuwa wapo hapa kusaidia Serikali ya Tanzania pamoja na Watu wake.

Wakati huo huo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan alikutana na kufanya Mazungumzo na Balozi wa Kenya nchi Mhe. Dan Kazungu ambaye alifika Ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha.

Mwisho Makamu wa Rais alikutana na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida ambaye amemaliza muda wake hapa nchi.

Makamu wa Rais alimshukuru Balozi Yoshida kwa ushirikiano wote alioutoa kwa kipindi chote alichokuwa hapa nchini.

Nae Balozi Yoshida aliishukuru Serikali ya Tanzania pamoja na watu wake kwa Ushirikiano mzuri waliompa kwa kipindi chake alichohudumu kama Balozi wa Japan hapa nchini.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA JENGO LA HOSPITALI YA MAMA NA MTOTO KIVUNGE UNGUJA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *