Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI Mhe.Selemani Jaffo akizungumza na Maafisa Utamaduni wa mikoa na Halmashauri zote nchini (hawapo katika picha) wakati akifunga Kikao Kazi cha Sekta hiyo kilichofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma.

MAAFISA UTAMADUNI KUONGEZEWA BAJETI – JAFO

  • Waziri   wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Seleman Jaffo amewaagiza Wakuu wa Mikoa  na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote nchini kuwawezesha Maafisa Utamaduni kwa kuwaongezea Bajeti itakayowawezesha kutimiza majukumu yao kwa ufasaha.
  • Agizo hilo amelitoa Jijini Dodoma wakati alipokuwa akifunga Kikao Kazi  cha  11 cha Maafisa Utamaduni kilichofanyika kwa siku mbili ambapo amewaagiza Wakurugenzi kutambua majukumu ya maafisa Utamaduni  ikiwemo kuhifadhi kuendeleza mila na desturi pamoja na kukuza lugha ya kiswahili.
SUSAN MLAWI
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Susan Mlawi. Akizungumza na Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote nchini (hawapo katika picha) wakati akifunga Kikao Kazi cha Sekta hiyo kilichofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma.
  • “Sekta hii ni muhimu sana kwakua ina wajibu wa kuelimisha na kuburudisha,hivyo naendelea kuwasitiza Wakurugenzi kuwawezesha Maafisa Utamaduni kushiriki katika kila Mkutano,kongamano,warsha zote zinazohusu sekta hiyo”.Alisema Mhe. Jaffo.
  • Aidha ameongeza kuwa thamani ya maafisa Utamaduni ni lazima ionekane kwakua ndio tasnia inayofundisha na kukuza Uzalendo hasa kujua alama,nyimbo na tunu za Taifa kwa vijana na wanafunzi nchini.
BAADHI YA MAOFISI
Baadhi ya Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri nchini wakifuatilia Kikao Kazi cha Sekta hiyo kilichofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma.
  • Katika hatua nyingine Mhe.Jaffo amewahakikishia Maafisa Utamaduni kuwa wavumilivu kuhusu muundo wa Kada hiyo ambapo amewaahidi kuwa suala hilo limepokelewa na Serikali itaanza mchakato wake ili kutatua changamoto hiyo.
  • Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Susan  Mlawi amesema kuwa Kikao Kazi hicho ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997 inayoeleza kuwa Wasimamizi na Watendaji wakuu wa shughuli za Utamaduni katika ngazi ya Taifa, Mkoa Wilaya na Taasisi za elimu na mafunzo kupata mafunzo ya uendeshaji ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao.
Kaimu Mkurugenzi
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bw.Boniface Kadili akitoa maelezo mafupi kuhusu ya Sekta yake wakati wa ufungaji wa Kikao Kazi cha Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote nchini kilichofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma.
  • “Kikao Kazi hiki kimepitisha maazimio yatakayokuwa mwongozo katika kuboresha utendaji wa Sekta hii ili kuimarisha utendaji kazi Ki-muundo na kisera baina ya maafisa Utamaduni wote waliopo Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI”.Alisema Bibi Susan.
  • Naye Afisa Utamaduni Wilaya ya Urambo Bw.Tito Lulandala ameeleza kuwa Sekta ya Utamaduni ina fursa nyingi zinazoweza kukuza pato la mwananchi mmoja na Taifa kwa ujumla katika nyanja mbalimbali ikwemo Michezo Sanaa na kukuza Utalii.
  • Katika kikao kazi hicho mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo Umuhimu wa Ubidhaishaji wa lugha ya kiswahili,Uhuishaji wa Sera ya Utamaduni,Sekta ya Filamu nyenzo muhimu katika kuimarisha Asili na Utamaduni
  • ,Fursa za utalii wa Kiutamaduni na nyinginezo.
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: HAFLA YA UAPISHO WA VIONGOZI WATEULE – IKULU DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 03 Febuari, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *