- Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amewataka waajiri wote nchini wenye wafanyakazi wa kigeni kuhakikisha kwamba Wafanyakazi hao wanawarithisha ujuzi Watanzania kwa mujibu wa sheria inavyoelekeza ili kuwajengea uwezo Watanzania na baadaye kutoa nafasi kwa Watanzania kushika nafasi hizo.
- Mavunde ameyasema hayo mkoani Arusha wakati akifanya ukaguzi katika Viwanda vya Sterling Surfancts,A to Z,Nethealth na Polyfoam mkoani Arusha ambapo alitumia fursa hiyo kuwataka Waajiri kusimamia kifungu cha 7 cha Sheria ya Uratibu wa Ajira kwa Wageni kinachomtaka kila mwajiri kuandaa mpango wa urithishaji wa Ujuzi kwa Wafanyakazi Watanzania kwa lengo la kuhakikisha Watanzania wananufaika na ujuzi huo.
- “Kama mwajiri atashindwa kutekeleza matakwa haya ya sheria,hii ni sababu inayojitosheleza kwa mamlaka kutokutoa vibali vya kazi kwa mwajiri mhusika kwa kushindwa kutekeleza Mpango wa Urithishaji Ujuzi”Alisema Mavunde
- Wakati huo huo Mavunde alipata nafasi ya kusikiliza kero za Wafanyakazi za kuhusu mikataba na malipo ya muda wa ziada ambapo alitoa maagizo kwa waajiri kuhakikisha ndani ya Siku thelathini(30) wanatatua changamoto hizo.
Ad